Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Jean Ping ajitangaza rais nchini Gabon ataka kura kuhesabiwa upya

Mzozo wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa nchini Gabon, wiki moja kamili tangu kufanyika kwa uchaguzi wa urais nchini humo na rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wiki hii.

Kiongozi wa upinzani nchini  Jean Ping, akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Septemba 2 2016 jijini Libreville
Kiongozi wa upinzani nchini Jean Ping, akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Septemba 2 2016 jijini Libreville STEVE JORDAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu watano wameuawa na maelfu kukamatwa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na jeshi la polisi jijini Libreville.

Aliyekuwa mgombea wa upinzani Jean Ping amejitangaza rais wa nchi hiyo na kudai kuwa yeye ndiye aliyeshinda.

Hatua hii inatarajiwa kuzua mgogoro zaidi wa kisiasa nchini humo katika siku zijazo.

Ping ambaye alikuwa amezuiliwa katika Makao makuu ya chama chake amesisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda na kueleza kuwa dunia inajua hilo.

"Kila mmoja duniani anafahamu nani ndio rais wa Jamhuri, ni mimi," amesema Ping.

Aidha, ametaka kura kuhesabiwa upya ili kubaini ukweli wa mambo kuhusu mshindi wa uchaguzi huo na kuitaka pia  Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati mzozo huo  haraka iwezekanavyo ili kumaliza machafuko yanayoshuhudiwa.

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu kinachoendelea nchini humo na kutaka uvumilivu kutoka pande zote mbili na kusikitishwa kwa machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.