Pata taarifa kuu
UN-GABAON

Umoja wa Mataifa watiwa wasiwasi na hali inayojri Gabon

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana Alhamisi hii Septemba 1 ili kuandaa programu yake ya Septemba, lakini kwa ombi la Ufaransa, mgogoro unaoendelea kushuhudiwa nchini Gabon ulitawala kikao hicho.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon au Burundi, ziarani Burundi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon au Burundi, ziarani Burundi. © REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Gabon inaweza kuwa chini ya majadiliano zaidi katika siku zijazo, kwani hali hiyo inatia wasiwasi Umoja wa Mataifa. Alhamisi Septemba 1, mjumbe wake maalum katika ukanda wa Afrika ya Kati, raia wa Senegal, Abdoulaye Bathily, aliwasilisha ripoti katika mkutano huo wa faragha.

Akiwa mjini Libreville kupitia technolojia ya kisasa, Alielezea hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Gabon na mlolongo wa matukio ya hivi karibuni, na kuungwa na wajumbe wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuendelea na kazi yake nchini humo. Kazi ambayo inamruhusu kuwasiliana moja kwa moja na pande zote mbili.

Makubaliano

Makubaliano yaliafikiwa katika mjadala huo na washiriki walitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kueleza kwa haraka wasiwasi wake na kukumbusha umuhimu wa mchakato wa uchaguzi uliouwazi na usio na upendeleo.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu, Balozi wa New Zealand Gerard van Bohemen, aliwatolea wito "wagombea wote, wafuasi wao, vyama vya siasa na wadau wengine kuwa watulivu, kukomesha vurugu au uchochezi wowote na kutatua migogoro ya aina yoyote kwa njia ya utaratibu wa kisheria na kikatiba. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.