Pata taarifa kuu
UFARANSA-GABON

Ufaransa yatiwa wasiwasi na kukosekana kwa raia wake Gabon

Ufaransa "haina taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake" baada ya machafuko makubwa yaliyofuata tangazo la kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Rais Ali Bongo nchini Gabon," Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema Jumatatu hii katika taarifa yake.

Maelfu ya wananchi wa Gabon wakiandamana mjini Paris dhidi ya uchaguzi uliyopelekea kuchaguliwa tena kwa Ali Bongo, huku waandamanaji wakibaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.
Maelfu ya wananchi wa Gabon wakiandamana mjini Paris dhidi ya uchaguzi uliyopelekea kuchaguliwa tena kwa Ali Bongo, huku waandamanaji wakibaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura. Thomas SAMSON / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Watu wengi wamekua wakikamatwa katika siku za hivi karibuni. Ufaransa haina taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake, " amesema Waziri, ambaye ameonyesha "wasiwasi wake mkubwa". Watu kadhaa, wenye uraia wa nchi mbili Ufaransa na Gabon hawajulikani walipo, chanzo cha kidiplomasia kumeliambia shirika la habari la AFP.

Vurugu zilizuka nchini Gabon baada ya kutangazwa kuwa Ali Bongo Ondimba ameshinda uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki moja iliyopita. Upinzani umeendelea kupinga matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani yanayompa ushindi Ali Bongo Ondimba.

Upinzani umeendelea kudai kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo vyote vya kura vya mkoa wa Haut-Ogooué, ambako inadhaniwa kuwa kura ziliibwa.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu, Balozi wa New Zealand Gerard van Bohemen, aliwatolea wito "wagombea wote, wafuasi wao, vyama vya siasa na wadau wengine kuwa watulivu, kukomesha vurugu au uchochezi wowote na kutatua migogoro ya aina yoyote kwa njia ya utaratibu wa kisheria na kikatiba. "

Machafuko nchini Gabon yamesababisha vifo vya watu zaidi ya saba na wengine wengi wamekamatwa na wengine hawajulikani waliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.