Pata taarifa kuu

AFCON: Mali imeilaza Afrika Kusini mabao 2 kwa 0

Nairobi – Timu ya taifa ya Burkina Faso, imeanza vema michuano ya kutafuta ubingwa taji la soka barani Afrika AFCON, inayoendelea nchini Cote Dvoire baada ya kuifunga Mauritania baoa 1 Kwa 0 kupitia mkwaju wa penalti, uliofungwa na Bertrand Traore aliyeipa ushindi timu yake katika dakika ya 96.

Leo ni zamu ya wawakilishi kutoka Afrika Mashariki, Tanzania itachuana na Morocco
Leo ni zamu ya wawakilishi kutoka Afrika Mashariki, Tanzania itachuana na Morocco REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Katika matokeo mengine, Namibia ilipata ushindi wa kihistoria wa bao 1 kwa 0 dhidi ya mabingwa wa zamani Tunisia, huku Mali nayo ikailaza Afrika Kusini mabao 2 kwa 0.

Leo ni zamu ya wawakilishi kutoka Afrika Mashariki, Tanzania itachuana na Morocco katika mechi ya kwanza ya kundi F saa 11 saa za Afrika Mashariki na baadaye DRC itamenyana na Zambia.

Mwandishi wetu Jason Sagini yupo mjini San Pedro, ametuma ripoti ifuatayo…

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.