Pata taarifa kuu

Algeria itafadhili tikiti za ndege za mashambiki wake kwa AFCON

Takriban mashabiki 2,000 wa Algeria wanaotaka kuhudhuria mechi za Fennecs wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Côte d'Ivoire watalipa 50% pekee ya gharama ya tikiti ya ndege, iliyosalia ikigharamiwa na Serikali, Shirikisho la Soka la Algeria (FAF) limetangaza.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria Baghdad Bounedjah akikabiliana na mchezaji wa Côte d'Ivoire Odilon Kossounou mnamo 2022.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria Baghdad Bounedjah akikabiliana na mchezaji wa Côte d'Ivoire Odilon Kossounou mnamo 2022. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais "Abdelmadjid Tebboune, ametoa maagizo ya kufidia 50% ya gharama za usafiri kwenda Côte d'Ivoire kwa mashabiki 2,000 (...), hatua inayoonyesha nia ya kuwaleta mashabiki karibu na timu yao wakati wa mechi zake", imetangaza FAF katika taarifa. FAF imemshukuru mkuu wa nchi wa Algeria kwa "mpango huu wa kusifiwa ambao unaonyesha uungaji mkono wake wa kudumu na usioyumba kwa timu ya kitaifa na mashabiki".

Maeneo ya mauzo yana hatari ya kuvamiwa na mashabiki wa dhati ambao watataka kupata mojawapo ya tikiti 2,000 zinazouzwa kwa nusu bei. Siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, kocha Djamel Belmadi alizindua orodha ya wachezaji 26 waliochaguliwa kutetea taifa la Algeria kwenye michunao ya AFCON, ambapo itacheza raundi ya kwanza kundi D pamoja na Angola, Burkina Faso na Mauritania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.