Pata taarifa kuu

Kiungo mshambuliaji wa Manchester Hannibal Mejbri kutoshiriki AFCON

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Hannibal Mejbri hayumo kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji wa Tunisia ambao watacheza Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Côte d'Ivoire kuanzia Januari 13 hadi Februari 11, 2024, iliyotangazwa Alhamisi na kocha Jalel Kadri.

Hannibal Mejbri wa Tunisia wakati wa Kombe la Kiarabu nchini Qatar mnamo Desemba 3, 2021.
Hannibal Mejbri wa Tunisia wakati wa Kombe la Kiarabu nchini Qatar mnamo Desemba 3, 2021. AP - Darko Bandic
Matangazo ya kibiashara

Akiwa na umri wa miaka 20 na akirejea kutoka Birmingham majira ya joto yaliyopita, Mejbri alicheza mechi tisa pekee katika mashindano yote tangu kuanza kwa msimu huu (bao moja, bila asisti) chini ya uongozi wa Erik ten Hag.

"Hannibal aliniambia kuwa hajisikii kuwa tayari kwa AFCON kwa sababu anapitia hali ngumu katika klabu," ameeleza Jalel Kadri katika mkutano na waandishi wa habari, kuhusu kiungo huyo ambaye amecheza mechi 27 na Carthage Eagles.

Wahbi Khazri wa klabu ya Montpellier (alicheza mechi 74, mabao 25) pia hatacheza AFCON baada ya kutangaza kustaafu soka ya kimataifa mnamo Desemba 2022.

Tunisia imeshinda michuano  hiyo mara moja tu, mnamo 2004 nyumbani.

Wachezaji wa Tunisia waliochaguliwa kwa AFCON:

Makipa (3): Aymen Dahmen (Al-Hazem/KSA), Mouez Hassen (Club Africain), Béchir Ben Said (US Monastir)

Mabeki: (9) Ali Abdi (Caen/UFARANSA/L2), Ali Maaloul (Al-Ahly/MISRI), Wajdi Kechrida (Atromitos Athens/UGIRIKI), Yassine Meriah (Espérance), Montassar Talbi (FC Lorient/UFARANSA), Hamza Jelassi (Etoile du Sahel), Yan Valery (Angers SCO/UFARANSA/L2), Oussama Haddadi (SpVgg Fürth/UJERUMANI/D2), Alaa Ghram (Sfaxien Sports Club).

Viungo (7): Elyes Skhiri (FC Cologne/UJERUMANI), Mohamed Ali Ben Romdhane (Ferencvaros/HUNGURY), Aïssa Laïdouni (Union Berlin/UJERUMANI), Houssem Teka (Espérance Tunis), Hamza Rafia (US Lecce/ITA), Mohamed Haj Mahmoud (FC Lugano), Anis Ben Slimane (Brøndby/DENMARK)

Washambuliaji (8): Youssef Msakni (Al-Arabi SC/QATAR), Naïm Sliti (Al-Ahli/QATAR), Taha Yassine Khenissi (Kuwait SC/KUWAIT), Haythem Jouini (Stade Tunisien), Seifallah Letaief (FC Winterthur/USWISI ), Bassem Serarfi (Klabu ya Afrika), Elias Achouri (FC Copenhagen/DENMARK), Mortadha Ben Ouanes (Kasimpasa SK/UTURUKI)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.