Pata taarifa kuu

Riadha: Mbio za Ethiopian Run kufanyika Jumapili

Nairobi – Na mwanaspoti wetu Paul Nzioki

Great Ethiopian Run
Ni mbio za kilomita 10 zinazofanyika Addis Ababa, kila Novemba © Great Ethiopian Run
Matangazo ya kibiashara

Toleo la 23 la Great Ethiopian Run linaanza Jumapili asubuhi katika mitaa ya Addis Ababa huku maandalizi ya mwisho yakiwa tayari yamekamilika kwa mashindano hayo ya kila mwaka. 

Tayari mbio za watoto zimefanyika kama sehemu ya kukamilisha maandalizi ya tukio rasmi, ambazo zilivutia zaidi ya washiriki 3500 na kauli mbiu ikiwa ni kukomesha polio miongoni mwa watoto. 

Great Ethiopian Run
Tayari mbio za watoto zimefanyika kama sehemu ya kukamilisha maandalizi ya tukio rasmi © Great Ethiopian Run

Meneja mkuu wa masoko wa Ethiopia Hilina Negussie amesema Polio imekuwa tishio nchini humo tangu kuanza kwa Uviko 19 na sehemu ya azimio lao mwaka huu ni kusaidia kuongeza ufahamu na fedha za kupambana na tishio hilo. 

"Tangu mlipuko wa Uviko 19, kesi za polio nchini zimekuwa nyingi na za kutisha. Tunataka kutoa elimu na ufahamu kwa wazazi kuwa njia pekee ya kupambana na polio ni chanjo." alisema Hilina Negussie.

Mwanzilishi mkuu wa mbio za Ethiopia na gwiji wa riadha Haile Gebraslasie
Mwanzilishi mkuu wa mbio za Ethiopia na gwiji wa riadha Haile Gebraslasie AFP/Archives

Mwanzilishi mkuu wa mbio za Ethiopia na gwiji wa riadha Haile Gebraslasie amesema mbio za watoto pamoja na mbio kuu zinalenga kuhamasisha kizazi kijacho cha wanariadha wa Ethiopia. 

Hizi ni mbio za kilomita 10 zinazofanyika Addis Ababa, kila Novemba.

Takriban washiriki 37000, 500 kati yao ni wanariadha wasomi na hivyo kulifanya kuwa tukio kubwa zaidi la riadha barani Afrika na ambalo linafahamika zaidi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.