Pata taarifa kuu

Morocco itakuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025

Morocco imetajwa kuwa nchi mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, uamuzi ambao lilitokana kwa kiasi fulani kukuza nia ya nchi hiyo na Uhispania na Ureno kuandaa Kombe la Dunia mnamo mwaka 2030, limetangaza Jumatano Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Senegal, mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2022, wakionysha kombe.
Senegal, mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2022, wakionysha kombe. © RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Toleo la 2027 litafanyika nchini Kenya, Uganda na Tanzania, amesema rais wa CAF Patrice Motsepe wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Cairo. Misri na Senegal pia walikuwa wametuma maombi. Shirikisho la Soka la Morocco limekaribisha "habari muhimu" kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) na kuongeza: "Mjitayarisheni kwa mashindano yasiyosahaulika".

Morocco itaandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza tangu 1988. Iliteuliwa kwa mwaka 2015 kabla ya kuomba kuahirishwa kutokana na kuenea kwa virusi vya Ebola. Lakini CAF hatimaye iliamua kuondoa hadhi hii na kuiondoa timu ya Morocco katika mashindano hayo, na nafasi yake ikachukuliwa na Equatorial Guinea.

Morocco iùenufaika wakati huu kutokana na kuondolewa kwa maombi mengine yote - Algeria, Zambia, maombi ya pamoja kutoka Nigeria na Benin -, amebainisha Patrice Motsepe.

"Sababu kuu ni kuunga mkono Morocco katika kuwania kwake Kombe la Dunia la 2030", kwa pamoja na Uhispania na Ureno, ameeleza rais wa CAF. "Kazi yetu ni kuhakikisha kuwa Afrika inaungana. Tumeamua kutoa kura 54 za bara la Afrika kwa Morocco," amesisitiza. Argentina, Uruguay, Paraguay na Chile ziliwasilisha ombi la pamoja la ushindani.

Afrika Mashariki yapewa nafasi

Hatua ya kuzipa Kenya ,Uganda na Tanzaniafursa hiyo inaipa Afrika Mashariki nafasi ya kwanza tangu 1976 kuandaa mechi hizo wakati Ethiopia ilipokuwa mwenyeji .

Kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, shirikisho pia "limeweka viwango vya juu sana katika suala la miundombinu". "Tuna uhakika kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi," Patrice Motsepe amesema. Kigezo kingine, AFCON haipaswi kupigwa mara mbili mfululizo katika eneo moja la Afrika, isipokuwa katika mazingira ya kipekee, amesema.

Mataifa ya Afrika Mashariki yalizishinda Misri, Senegal, Botswana na Algeria - ambao walijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho siku mbili kabla ya kutangazwa rasmi - kwa haki za kuandaa.

Katika jitihada hizo, Kenya inasemekana kuwa mbele ya uboreshaji wa Kituo cha Michezo cha Kimataifa cha Moi, Kasarani, na Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, huku Uwanja wa Kipchoge Keino mjini Eldoret, zaidi ya kilomita 300 kutoka mji mkuu, ikiwa ni chaguo la tatu.

Uganda inasemekana kutumia Uwanja wa Namboole .Haijulikani ni chaguo gani la pili na la tatu lilitolewa, au ni vifaa gani vya mafunzo vimeahidiwa.

Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa ulioidhinishwa na CAF tayari umetajwa kama utakaotumiwa nchini Tanzania. Chamazi Complex - makao ya Azam FC, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadhi ya viwanja vya Dodoma, Arusha na Zanzibar ni baadhi ya sehemu ambazo Tanzania italenga kuviboresha ili kukidhi viwango vya CAF.

Toleo lijalo, Afcon 2023, itafanyika nchini Ivory Coast, na litaanza Januari 13, 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.