Pata taarifa kuu

Kenya, Uganda na Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027

NAIROBI – Nchi za Kenya, Uganda na Tanzania zimeshinda katika ombi lao la kuwa wenyeji wa michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2027.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Patrice Motsepe akiidhinisha Kenya, Uganda na Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027, jijini Cairo Misri, Jumatano Septemba 27, 2023.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Patrice Motsepe akiidhinisha Kenya, Uganda na Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027, jijini Cairo Misri, Jumatano Septemba 27, 2023. © https://www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa na shirikisho la soka la Afrika CAF, ambapo pia nchi ya Morocco itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2025.

Mwaka wa 1996, Kenya ilipewa kibali cha kuwa mwenyeji wa mashindano hayo lakini baadaye ikanyaganywa baada ya kubainika kuwa baadhi ya viwanja havikuwa tayari.

Tayari viongozi wa ukanda wamezungumzia ushindi huu, kama anavyosema hapa rais wa Kenya William Ruto.

Watu wengi hawakuwa wanaamini kuwa tulikuwa na nafasi ya kuandaa AFCON 2027, kwa sasa tunahamasisha kila aina ya raslimali, tutahamasisha kila mtu na kila sekta kuhakikisha tunaandaa mashindano ya viwango vya dunia. Amesema Ruto.

Naye Michael Mwebe, mchambuzi wa masuala ya michezo akiwa nchini Tanzania amesifia hatua hii.

Ni hatua kubwa kwa ukanda wetu hatujawahi kuandaa mashindano makubwa kama haya ukizingatia kandanda au soka ndio mchezo unapendwa zaidi kwenye ukanda wetu na naamini wenzetu pia wamefurahi.

00:31

Michael Mwebe, mchambuzi wa michezo Tanzania 27 09 2023

Ombi hili la pamoja la mataifa ya Afrika Mashariki, limeidhinishwa na kamati tendaji ya CAF, na litakuwa la kwanza tangu Ethiopia kuandaa fainali za mwaka 1976.

 

Nchi ya Morocco ambayo itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwaka 2025, mara ya mwisho ilikuwa mwenyeji ni mwaka 1988.

Mwaka 2015 Morocco ilichaguliwa kuandaa mashindano hayo japo kutokana na virusi vya Ebola, taifa hilo liliomba mashindano yaahirishwa ingawa CAF baadaye iliamua kulipokonya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika haki ya kuwa mwenyeji.

Siku ya Jumanne Algeria ilijiondoa katika ya orodha ya wanaotaka kuandaa mashindano ya mwaka 2027.

Kujiondoa huku kunaweza kuelezewa na mbinu mpya kutoka kwa shirikisho la soka la Algeria, FAF, kuhusiana na mkakati wake wa kuendeleza soka nchini Algeria, ilisema.

Rais wa shirikisho hilo Patrice Motsepe amesema anajivunia Morocco, akisema nchini za Algeria, Zambia, Nigeria na Benin zilitangaza kujiondoa.

Lengo kubwa hapa ni kuiunga mkono Morocco katika  kugombea kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2030, kwa pamoja na Uhispania na Ureno, ameelezea Motsepe.

Morocco inajivunia viwanja vingi vya hadhi ya kimataifa na imefanikiwa kuandaa mashindano mengi ya soka ya Afrika na dunia.

Mashindano ya AFCON 2023 yatafanyika nchini Ivory Coast na yamesongeshwa mbele kutoka January hadi Februari 2024 kutokana na msimu wa mvua huko Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.