Pata taarifa kuu

UAE: Wachezaji na viongozi wa Kriketi washtakiwa kwa kupanga matokeo ya mechi

NAIROBI – Wachezaji nane wa kriketi na viongozi wameshtakiwa kwa kuenda kinyume cha sheria za ufisadi, katika uchunguzi wa mchango wao katika kuhitilafiana na mechi iliyoandaliwa ya T10 huko Abu Dhabi.

Nembo ya RFI Kiswahili
Nembo ya RFI Kiswahili © RFI Kiswahili
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa, Baraza La Kimataifa la Kriketi, ICC, kwa niaba ya Bodi ya Kriketi nchini humo, limesema mashtaka yanahusiana na Ligi ya Kriketi ya T10 ya Abu Dhabi ya 2021 na majaribio ya kupotosha mechi katika mashindano hayo.

Miongoni mwa walioshtakiwa ni Nasir Hossain mchezaji wa Bangladesh na wamiliki wenza wa timu hiyo Krishnan Kumar Chaudhary na Parag Sanghvi.

Mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kuhitilafiana na mechi, kuwapa wachezaji pesa ili kushiriki ufisadi na kudinda kushirikiana na baraza hilo la ICC katika uchunguzi.

Sita kati ya wale ambao wameshtakiwa wakiwemo Chaundary na Sanghvi, wamepigwa marufuku kwa muda kushiriki michezo na wana wiki mbili za kujibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.