Pata taarifa kuu

Soka: Roberto Mancini kuteuliwa kuwa kocha wa Saudi Arabia

Akijiuzulu katikati ya mwezi Agosti kutoka wadhifa wa kocha wa Italia, Roberto Mancini, kocha wa zamani wa Manchester City anatarajiwa kuteuliwa Jumatatu hii, Agosti 28, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Italia.

Kocha wa Italia Roberto Mancini wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Julai 5, 2021.
Kocha wa Italia Roberto Mancini wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Julai 5, 2021. Handout via REUTERS - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Italia, Roberto Mancini atajiunga na klabu mpya. Kocha huyo wa zamani wa Inter Milan au Manchester City ataanza kuinoa Saudi Arabia Jumatatu Agosti 28, kwa mujibu wa habari kutoka gazeti la kila siku la michezo la Italia La Gazzetta Dello Sport. Mancini, 58, ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka minne, hadi 2027, na Shirikisho la Soka la Saudi Arabia.

Atashiriki Jumatatu huko Riyadh mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari, linabainisha Gazeti hilo la kila siku la Italia, bila kutaja chanzo. Saudi Arabia, ambayo iliwashangaza wengi kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyopigwa nchini Qatar kwa kuiburuza Argentina ya Lionel Messi, bingwa wa dunia wa baadaye, mabao 2 kwa 1 katika hatua ya makundi, haikuwa na kocha tangu kuondoka kwa Mfaransa Hervé Renard, aliyeondoka kwenda kunoa wachezaji wa timu ta taifa ya wanawake ya Ufaransa.

Mshindi wa zamani wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya

Saudi arabia, nchi tajiri ilinunua majina ya wachezaji wakubwa nyota katika soka la dunia kama Cristiano Ronaldo, Karim Benzema au Neymar kwa matumaini ya kubadilisha taswira yake na kurekebisha uchumi wake. Mancini alihakikisha kwamba kujiuzulu kwake katika nafasi ya ukocha nchini Italia hakuhusiani na ofa kutoka Saudi Arabia na alikuwa amehalalisha hilo na maamuzi ya hivi karibuni ya mkuu wa Shirikisho la Italia (FIGC), Gabriele Gravina, hasa kuhusu muundo wa wafanyakazi wake.

"Kwa maoni yangu, hatukuwa tunaelewana tena," ameyaambia magazeti kadhaa ya kila siku ya Italia. "Kuna kitu kitakachotokea wakati kitu hiki kinanivutia, lakini Saudi Arabia haina uhusiano wowote jambo hilo. "

Chini ya uongozi wake, kuanzia Mei 2018 hadi Agosti 2023, Italia ilishinda Euro 2021 na kuweka rekodi ya michezo 37 bila kupoteza kati ya mwezi Septemba 2018 na Oktoba 2021.

Lakini La Nazionale pia walishindwa kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia la 2022, wakikosa fainali zao za pili mfululizo na hawakuanza vyema katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 nchini Ujerumani, wakipoteza nyumbani kwa England ( 2-1).

Alichaguliwa mara 36 (mabao 4) katika timu ya Italia. Maisha yake ya ukocha yalianza akiwa Fiorentina mwaka 2001, kabla ya kuiongoza Lazio Rome (2002-2004), Inter Milan (2004-2008 na 2014-2016) akiwa na mataji matatu ya ubingwa wa Italia, au Manchester City (2009-2013) ambayo aliiongoza 2012 hadi taji lake la kwanza la bingwa wa Uingereza kwa miaka 44.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.