Pata taarifa kuu

Kepa Arrizabalaga amejiunga na Real Madrid kwa mkopo

Nairobi – Real Madrid wamesajili mlinda lango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kwa mkopo kuchukua nafasi yake Thibaut Courtois ambaye anakabiliwa na changamoto ya jeraha.

Kepa Arrizabalaga, anachukua  nafasi yake Thibaut Courtois anayeuunguza jeraha
Kepa Arrizabalaga, anachukua nafasi yake Thibaut Courtois anayeuunguza jeraha © REUTERS/Antonio Tronic
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Real Madrid imesema imekubaliana na Chelsea FC kuhusu usajili wa Kepa Arrizabalaga hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka wa 2024.

Raia wa Ubelgiji Courtois, 31, atakosa mechi kadhaa za msimu huu kutokana na jeraha kwenye goti lake la kushoto.

Kepa, 28, alikuwa amehuishwa na klabu ya Bayern Munich, kabla ya kuamua kuelekea nyumbani kwao Uhispania.

Golikipa huyo wa zamani wa Athletic Bilbao alikuwa anakaribia kusajiliwa na klabu ya Real mwaka wa 2018 na baadae akaamua kujiunga na Chelsea kwa kima cha pauni milioni 71.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.