Pata taarifa kuu

Mbappe ameachwa nje ya kikosi cha PSG dhidi ya Lorient

Nairobi – Kylian Mbappe ameachwa nje ya kikosi cha Paris Saint-Germain kinachotarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya ufunguzi wa ligi wakati huu hatma ya mchezaji huyo kwenye klabu hiyo ikiwa haijulikani.

Mbappe, ambaye alikosa kushiriki mazoezi siku ya Ijumma ya wiki hii, amekataa kuongeza mkataba wake na mabingwa hao wa ligue 1
Mbappe, ambaye alikosa kushiriki mazoezi siku ya Ijumma ya wiki hii, amekataa kuongeza mkataba wake na mabingwa hao wa ligue 1 REUTERS - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Mbappe, ambaye alikosa kushiriki mazoezi siku ya Ijumma ya wiki hii, amekataa kuongeza mkataba wake na mabingwa hao wa ligue 1.

Suala la mkataba wa Mbappe limekuwa likizungumziwa pakubwa katika kipindi cha msimu huu wote.

Amekataa kusaini nyongeza ya mkataba wake na PSG, ikimaanisha kuwa anaweza kuondoka bure mwaka ujao, huku Real Madrid ikionekana kuwa lengo lake.

Inadaiwa kuwa Kylian Mbappé huenda akajiunga na Real Madrid
Inadaiwa kuwa Kylian Mbappé huenda akajiunga na Real Madrid REUTERS - GONZALO FUENTES

PSG wanataka kumuuza sasa ilikupata faida kubwa kwa ajili ya uhamisho wa mchezaji huyo aliyegharimu euro milioni 180 ($198m) kutoka Monaco mnamo 2017.

Mbappe hajaruhusiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza na alicheza mchezo mmoja tu kati ya tano za kujiandaa na PSG na hakualikwa kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Japan na Korea Kusini.

Klabu hiyo inaripotiwa kuwa tayari kumuuza nyota wa zamani wa Barcelona na kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, ambaye pia hajaitwa dhidi ya Lorient.

Luis Enrique, kocha mpya wa PSG
Luis Enrique, kocha mpya wa PSG REUTERS - GONZALO FUENTES

Huku Lionel Messi sasa akiwa na Inter Miami kocha mpya wa PSG Luis Enrique anatarajiwa kuanzisha washambuliaji watatu wapya wakiwemo raia wa Korea Kusini Lee Kang-In, Mreno Gonçalo Ramos na Mhispania Marco Asensio.

Mapema Jumamosi PSG walikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Barcelona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.