Rasmus Hojlund amesajiliwa rasimi na Manchester United
Nairobi – Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund kutoka Atalanta kwa ada ya pauni milioni 64 ($82 milioni) siku ya Jumamosi.
Imechapishwa:
Hojlund alikubali mkataba wa miaka mitano hii ikiwa ni mojawapo ya malengo ya meneja wa United Erik ten Hag kumsajili mshambuliaji kabla ya kampeni mpya ya Ligi Kuu ya Uingereza kuanza.
The stuff of dreams ❤️
— Manchester United (@ManUtd) August 5, 2023
Old Trafford, meet Rasmus Hojlund 🇩🇰#MUFC
"Sio siri kwamba nimekuwa shabiki wa klabu hii kubwa tangu nilipokuwa mdogo na nilikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa Manchester United," Hojlund alisema.
Rasmus Hojlund is a RED! ✍️🔴#MUFC
— Manchester United (@ManUtd) August 5, 2023
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anaweza kuigharimu United pauni milioni 8 zaidi ikiwa vipengele vya nyongeza katika mkataba wake vitatimizwa.
Ten Hag alimfanya Hojlund kuwa mlengwa wake mkuu baada ya United kuripotiwa kukataa kulipa bei iliyotakiwa na Tottenham kwa mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, ambaye anaonekana kuwindwa na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.
Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain walisemekana kuwa walikuwa wakiwinda saini ya Hojlund kabla ya United kushinda mbio hizo.