Pata taarifa kuu

Kombe la dunia: Afrika Kusini yaingia hatua ya 16 bora

Nairobi – Timu ya wanawake ya soka ya Afrika Kusini, imepata ushindi wao wa kwanza katika kombe la dunia baada ya kuifunga Italia kwa mabao 3-2 na kujikatia nafasi ya 16 bora.

Afrika kusini imejikatia nafasi katika hatua ya 16 bora
Afrika kusini imejikatia nafasi katika hatua ya 16 bora © FIFA Women's World Cup
Matangazo ya kibiashara

Nahodha Thembi Kgatlana alifunga bao la ushindi katika dakika ya 92 na kuweka historia kwa Afrika Kusini ambapo sasa watakutana na Uholanzi baada ya kuwaondoa Italia.

Kocha Desiree Ellis, ambaye timu yake ilifungwa 2-1 katika dakika za mwisho katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Sweden na kisha kutoka sare ya 2-2 na Argentina, amesema ushindi huu umewashngaza.

Kocha huyo amewasifia wachezaji wake kwa kujituma na kutokosa matumaini wakati wa mechi hiyo.

Timu hiyo imesema ushindi huu ni wa kila mtu nyumbani, watu ambao waliamka asubuhi na mapema ilikuwaunga mkono.  

Sweden imeongoza Kundi G kwa pointi tisa, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye pointi nne na Italia yenye pointi tatu. Argentina walimaliza wakiwa mkiani kwa bao moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.