Pata taarifa kuu

Mbappe hakujumuishwa kwenye kikosi cha PSG kinachozuru  Japan na Korea Kusini

Nairobi – Kylian Mbappe ameachwa nje ya kikosi cha Paris St-Germain kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Japan na Korea Kusini.

Kylian Mbappé ameonyesha nia yake ya kujiunga na Real Madrid
Kylian Mbappé ameonyesha nia yake ya kujiunga na Real Madrid © AFP - ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

Mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo amekataa kusaini nyongeza ya mwaka mmoja kwenye kandarasi yake itakayomalizika msimu ujao wa joto.

Kwa hivyo PSG wanataka kumuuza mshambuliaji huyo wa Ufaransa sasa na kupata ada ya uhamisho badala ya kumwacha aende bure.

Mbappe, hata hivyo, amesema anataka kubaki PSG kwa mwaka mmoja zaidi kabla ya kuondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa.

Anaaminika kuwa anataka kujiunga na Real Madrid bila malipo mwishoni mwa msimu ujao.

Kylian Mbappé anaaminiwa kuwa anataka kujiunga na Real Madrid
Kylian Mbappé anaaminiwa kuwa anataka kujiunga na Real Madrid AP - Christophe Ena

Mshambuliaji huyo anasalia kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi kuwahi kutokea, akijiunga na PSG mwaka 2017 kwa uhamisho wa thamani ya pauni milioni165.7.

Mshindi huyo wa kombe la dunia amefunga mabao 212 katika michezo 260 tangu atue kutoka AS Monaco.

PSG wanaamini hali ya sasa haiwezi kuruhusiwa kuendelea na kwa Mbappe kubaki kama sehemu ya kikosi chao, hivyo uamuzi wa kumuacha nyumbani.

Mwenyekiti Nasser Al-Khelaifi ameweka wazi azma yake ya kuchukua msimamo mkali juu ya suala hilo, akisema "haiwezekani" kwamba Mbappe ataruhusiwa kuondoka bure mnamo 2024.

Inafahamika kuwa vilabu kadhaa vimeulizia kuhusu Mbappe na PSG itakuwa tayari kumuuza msimu huu wa joto.

Kylian Mbappé, Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa
Kylian Mbappé, Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa © YVES HERMAN/REUTERS

PSG walishinda Ligue 1 msimu uliopita, lakini walimaliza kwa alama moja tu mbele ya RC Lens licha ya rasilimali zao nyingi za kifedha, na walitolewa nje ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya 16 bora na Bayern Munich.

Meneja Christophe Galtier aliondolewa kwenye nafasi yake mapema msimu huu wa joto na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Barcelona, ​​AS Roma na Uhispania Luis Enrique.

Lionel Messi tayari ameondoka Paris Saint-Germain
Lionel Messi tayari ameondoka Paris Saint-Germain AP - Michel Euler

Mshambuliaji mwingine nyota wa PSG, Lionel Messi, tayari ameondoka msimu huu wa joto.Raia huyo wa Argentina, ambaye nchi yake iliishinda Ufaransa ya Mbappe katika fainali ya kombe la dunia nchini Qatar Desemba mwaka jana, amejiunga na Inter Miami katika Ligi Kuu ya Soka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.