Pata taarifa kuu

Andre Onana kuitumikia Manchester Uinted kwa kipindi cha miaka mitano

Nairobi – Klabu ya Manchester United ya Uingereza imekamilisha usajili wa mlinda lango wa Cameroon Andre Onana kutoka Inter Milan ya Italia kwa euro milioni 51 ($57m).

Andre Onana amejiunga rasimi na Manchester United
Andre Onana amejiunga rasimi na Manchester United AFP
Matangazo ya kibiashara

Uhamisho uliotangazwa Alhamisi utamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kujiunga na United kwa kandarasi ya miaka mitano. Pia kuna chaguo la kuongeza mkataba huo kwa miezi 12 zaidi, na United italazimika kulipa euro milioni 4 ($4.5m) kama nyongeza, kulingana na mafanikio yake katika klabu hiyo.

"Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa, na nimefanya kazi kwa bidii maisha yangu yote kufikia wakati huu, kushinda vikwazo vingi njiani," Onana alisema.

Sasa ataungana na wachezaji wenzake wapya kwenye ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Onana anachukua nafasi ya David de Gea, ambaye alitangaza kuondoka United mwezi huu baada ya miaka 12 katika klabu hiyo.

Onana alitumia msimu mmoja tu Inter, ambapo alishinda Kombe la Italia na Kombe la Super. Pia aliisaidia klabu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Alirejeshwa nyumbani kutoka Kombe la Dunia mwaka jana nchini Qatar baada ya mzozo na kocha Rigobert Song. Baadaye alitangaza kuwa amemaliza kazi yake na timu ya taifa ya Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.