Pata taarifa kuu

CAF yaipongeza Morocco kwa mafanikio kwenye mchezo wa soka

Na: Paul Nzioki

Rais wa wa CAF Patrice Motsepe akiwa na viongozi wa soka nchini Morocco, Julai 07 2023
Rais wa wa CAF Patrice Motsepe akiwa na viongozi wa soka nchini Morocco, Julai 07 2023 © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Kamati Kuu ya Shirikisho la soka barani Afrika imetembelea makao makuu mapya ya shirikisho la soka Morocco FRMF na kufanya mkutano wake katika ofisi hizo zilizopo mjini Rabat.

 “Tuwapongeza kwa makao makuu mapya yenye hadhi ya Kimataifa,” alisema.

Mbali na hilo, CAF imewateuwa wajumbe wapya wafuatao kwenye Kamati ya Waamuzi ya CAF:

Kamati hio sasa itaongozwa na Hugues Alain Adjoyi kutoka Benin akisaidiwa na Makamu wa Rais Bw Victor Gomes kutoka Afrika Kusini.

Wanachama wengine ni:

Bi Fatou Gaye kutoka Senegal

Bw Dombouya Aboubacar kutoka Guinea

Bw Ali Mohammed Ahmed kutoka Somalia

Bi Tesfanesh Woreta kutoka Ethiopia

Bw Djamel Haimoudi kutoka Algeria

Bw Hadqa Yahya kutoka Morocco

Bw Olivier Safari Kabene kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Bw Louzaya René Daniel kutoka Kongo

Bw Inacio Candido kutoka Angola

Bi Gladys Lengwe kutoka Zambia

Bw Aminu Shantali Shuaibu kutoka Nigeria

Rais Motsepe aliongeza: “Uadilifu, uhuru na uaminifu wa waamuzi, makamishna wa mechi na waendeshaji VAR ni muhimu kwa heshima na ukuaji wa soka la Afrika na tuna imani kwamba wajumbe wapya wa Kamati ya Waamuzi wa CAF watachangia ukuaji na ushindani wa soka barani Afrika na kimataifa.”

Kamati ya Utendaji pia iliidhinisha kufutiliwa mbali kwa raundi ya pili ya Mtoano hili kufuzu katika katika mechi za Kombe la Shirikisho la CAF hatua ya makundi.

Hii ina maana kwamba Vilabu 16 vilivyoshinda Raundi ya Mtoano ya Awali ya Pili vitafuzu kwa Hatua ya Makundi katika mechi za kombe la shirikisho msimu wa 2023-2024.

Hapo awali timu zilizoshindwa kufuzu katika hatua ya makundi kwenye klabu bingwa zilikua zinapata nafasi ya kushiriki katika raundi ya pili ya kufuzu kwa hatua ya makundi katika kombe la shirikisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.