Pata taarifa kuu

Soka: Kylian Mbappé apokelewa kwa vifisho kwa ziara yake ya kwanza nchini Cameroon

Mshambulizi wa timu ya Ufaransa na Paris Saint-Germain amewasili siku ya Alhamisi, Julai 6 alasiri huko Yaoundé, ambapo umati wa watu wenye shauku ulimpokea kwa vifijo na nderemo. Kylian Mbappé, ambaye babake Wilfrid ni raia wa Cameroon, anakanyaga anawasili katika nchi hii kwa mara ya kwanza.

Mchezaji nyota Kylian Mbappé aakipokelewa na umati wa wawtualipowasili  kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Yaoundé, Cameroon mnamo Julai 6, 2023.
Mchezaji nyota Kylian Mbappé aakipokelewa na umati wa wawtualipowasili kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege wa Yaoundé, Cameroon mnamo Julai 6, 2023. AFP - DANIEL BELOUMOU OLOMO
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Yaoundé, Joël Wadem

Makundi kadhaa ya densi yalienda kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Yaoundé-Nsimalen mnamo Julai 6 kumpokea mmoja wa wanasoka bora zaidi ulimwenguni, kwa sauti ya midundo ya Cameroon. Takriban watu 2,000, wengi wao wakiwa vijana, pia walikuja kumwona Kylian Mbappé Lottin mwenye umri wa miaka 24 kwa mara ya kwanza.

"Kylian Mbappé ni mwanasoka, nataka kuwa kama yeye siku moja pia," anasema mmoja wao. "Ndoto yangu ni kumuona akiichezea Real Madrid", amesema mwingine.

"Ni furaha kubwa kumuona Kylian Mbappé kwa mara ya kwanza kwa macho yetu wenyewe, wakati tumezoea kumuona kwenye televisheni," amesema mmoja wa vijana hao. Mwingine anaongeza: “Ninajivunia kumuona. Kusema ukweli, nina furaha kubwa. "

Baada ya mwendo wa takriban dakika kumi, nahodha wa timu ya Ufaransa aliingia katika gari lake na kwenda, chuku akisindikizwa na ummati wa watu hadi kwenye Kijiji cha Noah. Hapa ndipo atatumia usiku wake wa kwanza na wa pili nchini Cameroon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.