Pata taarifa kuu

Rais wa CAF Motsepe aingilia kati mzozo wa timu ya wanawake ya Afrika Kusini

Nairobi – Na Paulo Nzioki

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF, Dr Patrice Motsepe
Rais wa shirikisho la soka barani Afrika, CAF, Dr Patrice Motsepe © CafOnline Media
Matangazo ya kibiashara

Rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF)  Patrice Motsepe, ameingilia kati kusuluhisha mzozo kati ya kikosi cha Afrika Kusini cha Kombe la Dunia la wanawake 2023 na chama cha kitaifa.

Rais Motsepe mwenye umri wa miaka 61 anatokea Afrika Kusini na anatarajiwa kufichua maelezo ya upatanishi wake mjini Johannesburg siku ya Jumatano.

"Mzozo huu unaohusisha timu ya wanawake ulikuwa aibu kubwa sio tu kwa Afrika Kusini, lakini Afrika nzima," kilisema chanzo cha CAF, ambacho kilizungumza kwa sharti la kutotajwa na shirika la AFP.

"Kuna kitu kilibidi kifanyike, Kwa haraka, huku baadhi ya wachezaji wa Afrika Kusini wakipangwa kuondoka kwenda New Zealand."

Rais wa CAF, Patrice Motsepe
Rais wa CAF, Patrice Motsepe © Pierre René-Worms

Australia na New Zealand wanashiriki Kombe la Dunia na mabingwa wa Afrika Afrika Kusini, Morocco, Nigeria na Zambia wanawakilisha bara la Afrika.

Tayari Motsepe amesaidia kutatua masuala yanayohusu kandarasi, ambayo wanachama wa kikosi walisema haikujumuisha ada ya kushiriki ya $30,000 (euro 27,500) iliyoahidiwa na FIFA kwa kila mmoja wa wachezaji 23.

Hii ilisababisha kikosi cha kwanza kutocheza mechi ya mtoano dhidi ya Botswana iliyopangwa kuchezwa Johannesburg Jumapili iliyopita, huku na kikosi cha pili kilichotajwa kwa haraka kikipoteza 5-0.

Banyana Banyana, The Girls of Kwazulu ikiwa ndio jina maarufu la timu ya taifa, pia hawakufurahishwa na uwanja huo, wakisema walihatarisha majeraha kwenye uwanja uliochukuliwa kuwa duni.

Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini
Timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini © Bafana Bafana

"Safa wanaweza kuhisi wamefanya vya kutosha, lakini nina maoni tofauti," mshambuliaji Jermaine Seoposenwe aliambia shirika la utangazaji la SABC.

“Lakini mwisho wa siku mimi ni mchezaji na kazi yangu ni kuja hapa, kucheza na kisha kuondoka,” aliongeza nyota huyo kutoka klabu ya Mexico ya CF Monterrey.

Wakiwa katika nafasi ya 54 duniani, Afrika Kusini wako ndani ya Kundi G, linalojumuisha washindi wa pili wa zamani wa Sweden (3), Italia (16) na Argentina (28).

Afrika Kusini itacheza na wenzao waliofuzu Costa Rica katika mechi ya kujiandaa na Julai 15 kabla ya kuanza kampeni ya Kombe la Dunia siku nane baadaye dhidi ya Wasweden huko Wellington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.