Pata taarifa kuu

Mason Mount amesajiliwa na Manchester United kutoka Chelsea

Nairobi – Manchester United imesajili kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount kutoka Chelsea kwa kima cha pauni  milioni 55 .

Mason Mount amesajiliwa na Manchester United kwa kipindi miaka mitatu
Mason Mount amesajiliwa na Manchester United kwa kipindi miaka mitatu REUTERS - DYLAN MARTINEZ
Matangazo ya kibiashara

Mount, ambaye alikubali kandarasi ya miaka mitano na Manchester, alisema "hawezi subiri kuwa sehemu ya harakati za wachezaji wa United kushinda mataji makubwa" huko Old Trafford.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alihitimu kutoka akademi ya vijana ya Chelsea na kucheza mechi 129 za ligi kuu ya Uingereza,  akifunga mabao 27.

"Si rahisi kamwe kuondoka katika klabu uliyokulia, lakini Manchester United itatoa changamoto mpya kwa awamu  inayofuata ya maisha yangu," Mount alisema.

"Baada ya kushindana dhidi yao, najua jinsi kikosi ninachojiunga nacho kilivyo imara, na siwezi kusubiri kuwa sehemu ya mpango wa kikosi hiki kushinda mataji makubwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.