Pata taarifa kuu

Kocha wa PSG anachunguzwa kwa tuhumza za ubaguzi akiwa Nice

Nairobi – Kocha wa Paris Saint Germain Christophe Galtier anazuiliwa kwa mahojiano pamoja na mwanawe kama sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya ubaguzi, mwendesha mashtaka wa Nice amethibitisha.

Kocha huyo anachunguzwa kwa tuhumza za kutoa matamshi ya kibaguzi wakati akiwa Nice
Kocha huyo anachunguzwa kwa tuhumza za kutoa matamshi ya kibaguzi wakati akiwa Nice AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inafuatia uchunguzi ulioanzishwa mwezi Aprili, kufuatia madai kwamba alitoa matamshi ya kibaguzi na chuki kuhusu wachezaji na kamati ya kiufundi alipokuwa meneja wa Nice msimu wa 2021/22.

Galtier anatarajiwa kuachishwa kazi na klabu na PSG kutokana na kile kinachotajwa kuwa klabu hiyo hakuonyesha mchezo wa viwango vya juu msimu uliopita ambapo walipoteza mechi 10 na kuondolewa katika mechi za kuwania klabu bingwa barani Ulaya katika awamu ya 16 bora.

Madai yanayomkabili yaliibuka katika vyombo vya habari nchini Ufaransa mwezi Aprili.

Christophe Galtier anatuhumiwa kutoa matamshi hayo akiwa na klabu ya Nice
Christophe Galtier anatuhumiwa kutoa matamshi hayo akiwa na klabu ya Nice AP - Thomas Padilla

Kwa mujibu wa tuhuma hizo ambazo hatukuweza kubainisha kama kituo, zinaeleza kuwa mwelekezi wa michezo katika klabu ya Nice , Julien Fournier alikuwa ameandika barua pepe kuelekea mwishoni mwa msimu wa 2021/22 ikiwa na madai kuwa Galtier alikuwa ametoa matamshi ya kibaguzi kwa wanachama wa klabu ya Nice .

Fournier anadai kuwa kocha huyo alimfahamisha kwamba hawafai kuwa na wachezaji wa kiafrika wa wale wa dini ya Kiisilamu  kwenye kikosi ambapo alihitaji kufanya mageuzi kupunguza idadi ya wachezaji waisilamu.

Galtier na Fournier waliondoka katika klabu ya Nice mwaka jana baada ya kuhudumu kwa msimu mmoja peke kabla ya Galtier kupewa majukumu na PSG.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.