Pata taarifa kuu

N'Golo Kante ni mchezaji wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia

NAIROBI – Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante amekubali kujiunga na mabingwa wa Saudi Arabia Al-Ittihad.

N'Golo Kante amejiunga na klabu ya Al-Ittihad ya nchini Saudi Arabia
N'Golo Kante amejiunga na klabu ya Al-Ittihad ya nchini Saudi Arabia AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 nchini Uingereza katika klabu ya Chelsea, unatarajiwa  kukamilika mwishoni mwa Juni mwaka huu.

Kante amekuwa akikabiliwa na majeraha na aliichezea Chelsea mechi tisa peke katika msimu wa  2022-23.

Kwa sasa mchezaji huyo ataungana na Karim Benzema katika klabu ya Al-Ittihad baada ya Mfaransa mwenzake kuondoka Real Madrid na kusaini mkataba wa miaka mitatu mwezi huu.

Karim Benzema  alijiunga na Al Ittihad ya nchini Saudi Arabia
Karim Benzema alijiunga na Al Ittihad ya nchini Saudi Arabia via REUTERS - Al Ittihad

Hatua hiyo inahitimisha kipindi cha mafanikio makubwa katika soka la Uingereza kwa Kante.

Aliisaidia Leicester City kushinda ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2015-16 kabla ya kuhamia Stamford Bridge. Akiwa Chelsea Kante alishinda klabu bingwa barani Ulaya, ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, ligi ya Uropa na kombe la FA.

N'Golo Kante alikuwa na mafaniko wakati akiwa Chelsea kabla ya kukabiliwa na majeraha
N'Golo Kante alikuwa na mafaniko wakati akiwa Chelsea kabla ya kukabiliwa na majeraha AFP

Aliteuliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Chama cha Waandishi wa Soka na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji Soka kwa 2016-17.

Pia alitekeleza jukumu muhimu wakati Ufaransa iliposhinda Kombe la Dunia mnamo 2018.

Ngolo Kanté alkuwa na mchango mkubwa wakati timu ya taifa ya Ufaransa iliposhinda ubingwa wa kombe la dunia
Ngolo Kanté alkuwa na mchango mkubwa wakati timu ya taifa ya Ufaransa iliposhinda ubingwa wa kombe la dunia AFP

Kante amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo wenye thamani ya £86m.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.