Pata taarifa kuu

Chelsea imemsajili mshambuliaji wa Ufaransa Nkunku kutoka RB Leipzig

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Christopher Nkunku wa RB Leipzig, ameihamia Chelsea ya Uingereza
Christopher Nkunku wa RB Leipzig, ameihamia Chelsea ya Uingereza REUTERS - MATTHIAS RIETSCHEL
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Chelsea ya England imekamilisha usajili wake wa fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 63 ($80 milioni) siku ya Jumanne.

Nkunku tayari alikuwa amekubali kandarasi ya awali na klabu hiyo ya Ligi Kuu nchini Engalnd mwezi Desemba na sasa ameweka ametia saini makubaliano ya kuhamia Stamford Bridge.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameweka bayana kuhusu kandarasi ya miaka sita yenye faida kubwa na The Blues, ambao wanaanza ukarabati wa msimu mpya huku wakitarajia kurejea kutoka kwa kampeni mbaya ya msimu uliopita.

Christopher Nkunku  amekubali kuhamia Chelsea akitokea Leipzig
Christopher Nkunku amekubali kuhamia Chelsea akitokea Leipzig POOL/AFP

"Chelsea ina furaha kutangaza Christopher Nkunku atajiunga na klabu hiyo kutoka RB Leipzig kabla ya msimu wa 2023/24," taarifa kwenye tovuti ya Blues ilisema.

Nkunku ni mmoja wa nyota wanaochipukia katika soka la Ulaya na alifunga mabao 23 katika michezo 36 aliyoichezea Leipzig msimu uliopita.

Ni mchezaji wa kwanza mwenye tajiriba kusajiliwa tangu Mauricio Pochettino kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa Chelsea mwishoni mwa Mei.

"Nina furaha sana kujiunga na Chelsea. Juhudi kubwa ilifanywa kunileta katika klabu," Nkunku alisema.

"Natarajia kukutana na kocha wangu mpya na wachezaji wenzangu na kuwaonyesha wafuasi wa Chelsea kile ninachoweza kufanya uwanjani."

Nkunku, alihitimu kutoka akademi ya soka ya kitaifa ya Ufaransa huko Clairefontaine, alikaa miaka minne Paris Saint-Germain kabla ya kuhamia Leipzig mnamo 2019.

Christopher Nkunku aliwahi kuichezea  PSG
Christopher Nkunku aliwahi kuichezea PSG AFP/Archives

Alijitambulisha na klabu hiyo ya Ujerumani na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Bundesliga msimu wa 2021-22 baada ya kufunga mabao 20 na kutoa asisti 15 kwenye ligi.

Mshambulizi huyo mwenye uwezo mkubwa alifunga mabao 23 zaidi msimu huu na kuisaidia Leipzig kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Bundesliga na kufunga bao katika ushindi wao wa fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.