Pata taarifa kuu

Waamuzi Kutoka Misri Kusimamia mechi ya Taifa Stars dhidi ya Niger kufuzu AFCON

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania
Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania © Taifa stars
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka nchini Misri kusimamia mechi ya  kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Niger.

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa saa kumi jioni, hapo kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa CAF, mwamuzi wa kati atakuwa Mohamed Al Sayd, ambaye atasaidiwa na Youssef Elbosaty na Samy Halhal. Afisa wa nne, au mwamuzi wa akiba ni Mahmoud Nagi.

Taifa Stars wamo Kundi F, wakipambana kupata nafasi ya kuungana na Algeria ambao tayari wamefuzu kwa fainali za AFCON zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Algeria hadi sasa imekusanya pointi 12 ambazo hazitafikiwa na nchi nyingine tatu kwenye kundi hilo.

Vinara wa kundi hilo watakutana na Uganda katika pambano la ugenini lililopangwa kufanyika katika Uwanja wa Japoma mjini Douala, Cameroon.

Uganda wameamua kutumia uwanja wa Cameroon kwa sababu viwanja vyao vingi havikidhi matakwa ya CAF kwani katika mechi yao dhidi ya Taifa Stars, waliamua kutumia Uwanja wa Ismailia wa Misri.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amouroche sasa anawanoa wachezaji wake ambao watakuwa chini ya Nahodha Mbwana Samatta na Saimon Msuva.

Taifa Stars inashika nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi nne katika mechi nne.

Kocha wa Taifa Stars- Adel Amouroche
Kocha wa Taifa Stars- Adel Amouroche © Taifa stars

Uganda wanashika nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya pointi sawa na Tanzania na Niger walio mkiani wakiwa na pointi mbili.

Kimsingi, Tanzania, Uganda na Niger zina nafasi ya kuungana na Algeria kwa ajili ya fainali hizo ikiwa ni kuandikisha matokeo ya kuvutia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.