Pata taarifa kuu

Tennis: Morocco yatinga fainali ya Billie Jean King Cup 2023

Na: Jason Sagini

Mchezaji wa Morocco Aya El Aouni
Mchezaji wa Morocco Aya El Aouni © Tennis Kenya
Matangazo ya kibiashara

Kwenye siku ya tano ya mashindano ya Billie Jean King Cup jijini Nairobi nchini Kenya, Morocco wamemaliza nafasi ya kwanza kwenye Kundi A kwa alama nne na hivo basi kufuzu fainali dhidi ya Tunisia hapo kesho kuwania tiketi moja tu ya kupandishwa daraja hadi la pili barani Afrika.

Hii ni baada ya Kenya kupoteza mechi mbili leo dhidi ya Nigeria.  Angella Okutoyi alimlaza Adesuwa Osabuohien seti 2-0 za 6-2, 6-0 ila Cynthia Cheruto akapoteza 2-0 za 6-0, 6-2 dhidi ya Barakat Oyinlomo na kwenye mechi ya wachezaji wawili kila upande, Okutoyi na Cheruto wakapoteza 2-0 za 6-1, 6-2 dhidi ya Oyinlomo na Dasam Nweke. 

Leo uwanja ulikua na kelele sana na tulitarajia. Lakini tulikuja kutafuta ushindi haswa baada ya kupoteza mechi zote jana dhidi ya Morocco, alisema mchezaji wa Nigeria Barakat Oyinlomo. 

Kocha wa Kenya Francis Rogoi amepongeza juhudi za timu ya Kenya akisema wamejitahidi zaidi kuliko mashindano yaliyopita. Mwaka jana Kenya ilimaliza nafasi ya 11. Kenya itachuana na Zimbabwe kesho kuwania nafasi ya tatu. 

"Nahisi vizuri tumefika fainali. Kenya hawakubahatika leo. Michezoni lazima kuwe na mshindi na mshindwa," alisema kocha wa Morocco Att Barhouch Mehdi.  

Aya El Aouni mchezaji wa Morocco
Aya El Aouni mchezaji wa Morocco © Tennis Kenya

Mshindi wa mechi ya Morocco na Tunisia ataiwakilisha Afrika katika michuano ya Euro-Afrika msimu ujao. 

"Dhidi ya Tunisia tutajituma tena zaidi, tunaufahamu mchezo wao tayari kwa hivyo haitakua mechi ngumu," Mehdi alisisitiza baada ya kushinda mechi zao zote tatu dhidi ya Botswana.  

Kesho ikiwa siku ya mwisho ya mashindano, Uganda watapambana na Ushelisheli kuwania tiketi ya kuepuka kushuka daraja baada ya wote kumaliza nafasi ya mwisho kwenye makundi. Burundi watasalia kwenye daraja hili la tatu kwani wamemaliza nafasi ya tano kwenye kundi B. 

Tunisia imemaliza kwa alama tano bila ya kupoteza mechi yoyote mbele ya Zimbabwe. Ghana na Mauritius ni za tatu na nne mtawalia.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.