Pata taarifa kuu

Tennis: Kenya yailemea Uganda mashindano ya Billie Jean King

Na: Jason Sagini

Cynthia Cheruto mchezaji wa Kenya
Cynthia Cheruto mchezaji wa Kenya © Tennis Kenya
Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Afrika Mashariki  Uganda, Kenya na Tanzania  mara nyingi zinapokutana kwenye michezo huzingatiwa kama debi lenye uhasama mkubwa. Mwaka 2019 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mchezo wa soka, Kenya ilitoka nyuma na kuishinda Tanzania mabao 3-2 kwenye makundi ila wote waliyaaga mashindano kwenye hatua hiyo.  

Mwaka 2021, Kenya na Uganda zilitoka sare ya 1-1 jijini Kampala na 0-0 jijini Nairobi katika mechi za kufuzu kombe la dunia la mwaka 2022. 

Uhasama huo umeshuhudiwa leo katika uwanja wa Nairobi Club katika mashindano ya tenisi Kombe la Dunia barani Afrika daraja la tatu kwa kina dada, ambapo Kenya ilifanikiwa kuishinda Uganda mechi zote tatu kwenye kundi A. 

Angella Okutoyi alitumia dakika 36 tu kumlaza Patience Athieno seti 2-0 za 6-0, 6-0 naye Cynthia Cheruto akamshinda Winnie Birungi seti 2-0 za 6-3, 6-0.

Kwenye mechi ya wachezaji wawili kila upande Roselida Asumwa na Mellisa Mwakha mwenye makaazi yake nchini Zimbabwe wakawashinda Patience Athieno na Winnie Birungi seti 2-0. 

Si mara ya kwanza kucheza nao. Kucheza nao kwao ni ngumu sana sababu ya mashabiki. Wachezaji wao wana uzoefu kuliko wetu ila tunaendelea kujifunza, alisema kocha wa Uganda Edward Odokcen. 

Barakat Oyinlomo Quadre mchezaji wa Nigeria akipambana kwenye mchuano muhimu, Juni 14 2023
Barakat Oyinlomo Quadre mchezaji wa Nigeria akipambana kwenye mchuano muhimu, Juni 14 2023 © Tennis Kenya

Kenya imesalia na mechi mbili dhidi ya Namibia na viongozi wa kundi A Nigeria. Uganda ingali inavuta mkia bila ushindi wowote hadi sasa kabla ya kupambana na Botswana kisha Namibia. 

Kuishinda Uganda inatuongeza motisha kabla ya kupambana na Nigeria. Lazima tungeshinda,  alisema Cynthia Cheruto mchezaji wa Kenya.  

Kocha wa Nigeria, Rotmi Akinloye, amesifia ukuaji wa mchezo huo katika ukanda wa Afrika Mashariki akisema Kenya inaonekana kuwa taifa bora zaidi kwenye mashindano ya Billie Jean King Cup ya mwaka huu. 

Kenya waliweka historia ya Wimbledon kupitia Angella Okutoyi mwaka 2022 . Burundi wangefanya vizuri zaidi ila hawakuja na mchezaji wao bora. 

Mashirikisho yenu yanastahili kuwekeza zaidi katika ukuzaji talanta. Hili litaboresha nafasi zenu kwenye msimamo wa dunia,  kocha Rotmi Akinloye.  

Burundi leo imepoteza mechi zote tatu dhidi ya viongozi wa kundi A Tunisia ambao kama tu Nigeria, hawajapoteza mechi yoyote hadi sasa.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.