Pata taarifa kuu

Mbappe hataongeza mkataba wake na PSG

NAIROBI – Klabu ya Paris St-Germain ya nchini Ufaransa huenda ikaamua kumuuza mchezaje wake Kylian Mbappe msimu huu wa joto badala ya hatari ya kumpoteza bila malipo katika muda wa mwaka mmoja, hatua hii ikija baada ya mchezaji huyo kuiambia klabu hiyo kuwa hataongeza mkataba wake.

Kylian Mbappe ameiambia PSG kuwa hataongeza mkataba wake na klabu hiyo
Kylian Mbappe ameiambia PSG kuwa hataongeza mkataba wake na klabu hiyo AP - Francois Mori
Matangazo ya kibiashara

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu ujao akiwa na chaguo  la kuongeza mwaka mwingine katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, kulikuwepo  na makataa ya Julai 31 kwa Mbappe, 24, kuiambia PSG iwapo alikuwa anawazia kufanya mkataba wake upya  hadi mwaka wa 2025.

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, mchezaji huyo ameitumia klabu hiyo barua akisema hatofanya hivyo.

Mfungaji huyo bora wa PSG atakuwa huru kuondoka bila malipo mwishoni mwa msimu ujao na hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya kufanya mazungumzo.

Kylian Mbappé amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu yake ya Paris Saint-Germain.
Kylian Mbappé amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu yake ya Paris Saint-Germain. © AFP - ALAIN JOCARD

Hata hivyo, wakati mabingwa hao wa Ufaransa wakijaribu kurekebisha sera ya michezo kwa timu yao baada ya miaka mingi ya kununua wachezaji nyota bila mkakati madhubuti, PSG wameazimia kutomwacha Mbappe kwenda bure, huku klabu hiyo ikikerwa na barua ya mchezaji huyo iliyovujishwa kwenye vyombo vya habari kwanza kabla ya wao kuiona.

Ina maana kwamba wasipopata hakikisho kuhusu nia ya baadaye ya mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018, watamuuza katika hatua ambayo itaweka vilabu vinavyoongoza barani Ulaya kuwa macho.

Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid
Wachambuzi wa michezo wanasema kuwa huenda Mbappe akachukua nafasi ya Karim Benzema aliyeondoka Real Madrid AP - Bernat Armangue

Real Madrid wamekuwa wakitaka huduma za Mfaransa huyo kwa muda mrefu na alikataa kuhamia Bernabeu kusalia PSG mwaka jana.

Kuondoka kwa Karim Benzema kuelekea nchini Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real inahitaji mshambuliaji, ingawa inamwazia mchezaji wa Tottenham kuwa Harry Kane.

Harry Kane amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid
Harry Kane amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid REUTERS - ANNEGRET HILSE

Mbappe, ambaye alijiunga na PSG mwaka 2017 kwa mkopo akitokea Monaco kabla ya uhamisho wa euro 180m na amefunga mabao 212 katika michezo 260.

Ana mabao 38 katika mechi 68 alizoichezea Ufaransa, ikiwa ni pamoja na mabao matatu kwa mpigo katika fainali ya mwaka jana nchini Qatar, Ufaransa iliposhindwa na Argentina kwa mikwaju ya penalti.

Mbappe alikuwa na mchango mkubwa kwa klabu yake wakati wa kombe la dunia nchini Qatar
Mbappe alikuwa na mchango mkubwa kwa klabu yake wakati wa kombe la dunia nchini Qatar AP - Hassan Ammar

Mbappe alimaliza kama mfungaji bora wa Ligue 1 katika kila misimu mitano iliyopita na ameshinda mataji matano ya ligi katika misimu yake sita akiwa PSG.

PSG ilimaliza msimu wa 2022-23 kwa kutwaa taji la Ligue 1 pekee baada ya kushindwa tena kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, na kufungwa na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora.

Bayern waliwaondoa Paris St Germain katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya
Bayern waliwaondoa Paris St Germain katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya REUTERS - ANGELIKA WARMUTH

Mbappe atakuwa mshambuliaji wa pili mwenye hadhi ya juu kuondoka Parc des Princes msimu huu, baada ya mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kuondoka mwishoni mwa kandarasi yake ya miaka miwili na kujiunga na Inter Miami ya Ligi Kuu ya Soka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.