Pata taarifa kuu

Al Ahly wameshinda taji la klabu bingwa barani Afrika mara kumi na moja

NAIROBI – Timu ya Al Ahly ya Misri imeshinda Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya 11 rekodi.

Al Ahly wameshinda taji la klabu bingwa barani Afrika
Al Ahly wameshinda taji la klabu bingwa barani Afrika REUTERS - ABDELHAK BALHAKI
Matangazo ya kibiashara

Al Ahly ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Wydad Casablanca katika mechi ya mkondo wa pili nchini Morocco, na kupata ushindi wa jumla wa 3-2.

Mohamed Abdelmoneim wa Al Ahly alifunga bao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika 13.

Wydad walikuwa wamewashinda wapinzani wao wakubwa Al Ahly wakati walipokutana mwaka jana mjini Casablanca.

Ligi ya mabingwa barani Afrika kwa miongo kadhaa imekuwa ikitawaliwa na vilabu vya Afrika Kaskazini.

Timu kutoka kanda hiyo zimeshinda matoleo 16 kati ya 23 zilizopita za mashindano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.