Pata taarifa kuu

Fainali ya klabu bingwa barani Afrika, Al Ahly dhidi ya Wydad AC

NAIROBI – Al Ahly watakuwa wakitafuta nafasi ya kupata ubingwa wa Afrika tena watakapomenyana na mabingwa watetezi Wydad AC katika mkondo wa pili wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Al Ahly kucheza dhidi ya Wydad Casablanca kuwania ubingwa wa Afrika
Al Ahly kucheza dhidi ya Wydad Casablanca kuwania ubingwa wa Afrika REUTERS - AMR ABDALLAH DALSH
Matangazo ya kibiashara

Fainali hii ni marudio ya mwaka jana, baada ya Wydad AC kushinda fainali ya mwaka jana walipokutana katika fainali ya mkonodo mmoja. 

Kocha wa Wydad Sven Vandenbroeck baada ya mchezo wa kwanza kule Misri alisema kuwa yuko tayari kuitumia vizuri fainali ya pili akiwa nyumbani. 

Baada ya fainali tatu za mechi moja kuanzia 2020, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limerejea kwa uamuzi wa mikondo miwili msimu huu. 

Rais wa CAF  Patrice Motsepe
Rais wa CAF Patrice Motsepe AP - Themba Hadebe

Rekodi Kuelekea Fainali 

Ikiwa Ahly, wanaongoza kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya mkondo wa kwanza, wakishinda mkondo wa pili watakua mabingwa wa kwanza kushinda mechi 10 kwa msimu mmoja. 

Ahly (mara tatu), Wydad, Esperance ya Tunisia, TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Enyimba ya Nigeria zimefanikiwa kupata ushindi mara tisa kila moja. 

Enyimba na Raja Casablanca wana rekodi ya kunyanyua kombe hilo baada ya kushinda mechi tano pekee kila moja. 

Kocha wa Mreno Manuel Jose anashikilia rekodi ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa, akiiongoza Ahly kushinda mwaka wa 2001, 2005, 2006 na 2008. 

Mashabiki wa Wydad Casablanca
Mashabiki wa Wydad Casablanca AFP - -

Jukumu lake limerahisishwa aliposimamia kikosi cha Ahly cha 2005-2008 ambacho kinachukuliwa kuwa chenye nguvu zaidi katika historia ya vilabu barani Afrika. 

Wydad walipata kichapo cha nne msimu huu walipopoteza mechi ya kwanza ya fainali mjini Cairo, na kufikia rekodi ya kupoteza mara nyingi zaidi kutoka kwa klabu iliyonyakua taji la Ligi ya Mabingwa. 

Wydad pia walipoteza mara nne mwaka wa 2017 waliposhinda shindano hilo kwa mara ya pili kwa kuwalaza Ahly kwa jumla ya mabao 2-1. 

Wachezaji wa Al Ahly
Wachezaji wa Al Ahly AP

Nani Wanaotafuta Historia Katika Fainali Hii 

Kiungo wa kati wa zamani Vandenbroeck, 43, anamatumaini ya kuwa Mbelgiji wa kwanza kufundisha timu na kushinda taji la Ligi ya Mabingwa ya CAF. 

Wamorocco Hussein Ammouta na Walid Regragui na Yuriy Sevastyanenko wa Ukraine waliifundisha Wydad na kupata ushindi katika mashindano ya kwanza ya vilabu vya Afrika. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.