Pata taarifa kuu

Ujio wa Messi Inter Miami waiongozea wafuasi kwenye mitandao ya kijamii

NAIROBI – Mkataba unaokuja wa Lionel Messi na Inter Miami umezua msisimko miongoni mwa mashabiki wa nyota huyo wa kandanda wa Argentina, idadi kubwa ya watu kwenye mitandao ya kijamii na mauzo ya tikiti yakiongezeka.

Lionel Messi, anatarajiwa kusaini mkataba na Inter Miami ya Marekani
Lionel Messi, anatarajiwa kusaini mkataba na Inter Miami ya Marekani REUTERS - KAI PFAFFENBACH
Matangazo ya kibiashara

Wakati Messi bado hajasaini mkataba huo, wafuasi wa Inter Miami kwenye Instagram waliongezeka mara nne tangu mshindi huyo wa Kombe la Dunia alipofichua Jumatano kwamba ataelekea katika klabu ya Ligi Kuu ya Soka baada ya kuondoka Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Akaunti ya Inter ilikuwa na takriban wafuasi 900,000 kabla ya Jumatano. Chini ya saa 24 baada ya habari hiyo kusambaa, idadi hiyo ilikuwa imefikia wafuasi milioni 5.7.

Sasa ina wafuasi zaidi ya milioni 7.5 kwenye majukwaa yote ya kijamii na iliongeza zaidi ya wafuasi wapya milioni tano wakati tangazo hilo lilipofanyika.

Messi aliisaidia timu yake ya taifa kushinda kombe la dunia mwaka wa 2022
Messi aliisaidia timu yake ya taifa kushinda kombe la dunia mwaka wa 2022 AP - Martin Meissner

Bei ya wastani ya mechi za nyumbani za Inter Miami iliongezeka kutoka $31 hadi $152 huku kwa michezo ya ugenini iliongezeka kutoka $94 hadi $207, kampuni ya tiketi ya Logitix imesema.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alikatiza matumaini ya kuungana tena na klabu hiyo ya Uhispania ambapo aliimarika kwa takriban miongo miwili kabla ya kuondoka na kujiunga na PSG.

Leo Messi amewambia wanahabari kuwa alifanya uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo ya Marekani
Leo Messi amewambia wanahabari kuwa alifanya uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo ya Marekani REUTERS - CARL RECINE

Barcelona ilizama kwenye deni wakati Messi alipoondoka mwaka 2021, na alilazimika kusubiri kwa matumaini ya kuongezewa mkataba wake. Raia huyo wa Argentina inaonekana alitaka kurejea lakini "hakutaka kuwa katika hali hiyo tena", aliviambia vyombo vya habari vya Uhispania.

Messi mwenye umri wa miaka 35, alichagua kujiunga na Inter Miami  licha ya kuripotiwa kuwa na ofa nono zaidi kutoka Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.