Pata taarifa kuu

Elena Rybakina ajiondoa kwenye mashindano ya French Open

NAIROBI – Mchezaji nambari nne kwa ubora duniani na bingwa wa Wimbledon Elena Rybakina amejiondoa kwenye michuano ya French Open akikabiliwa na "homa".

Bingwa wa Wimbledon Elena Rybakina amejiondoa kwenye michuano ya French Open
Bingwa wa Wimbledon Elena Rybakina amejiondoa kwenye michuano ya French Open © Pierre Rene-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Rybakina alikuwa amepangwa kukutana na Sara Sorribes Tormo wa Uhispania katika raundi ya tatu.

"Nilikuwa sijisikii vizuri jana na juzi. Sikulala jana usiku," alisema Rybakina.

"Nilikuwa na homa na maumivu ya kichwa na ni vigumu kupumua. Nilijaribu kujiweka kwenye sehemu ya joto lakini ninahisi ni uamuzi sahihi kujiondoa."

Hatua yake ya kujiondoa kwa sababu ya maumivu kunatoa nafasi kubwa kwa bingwa mtetezi Iga Swiatek kushinda taji hilo.

iga swiatek
iga swiatek © Pierre René-Worms

Rybakina amesema kwa sasa anaangazia namana ya kurejea katika afya nzuri kabla ya kutetea taji lake kwenye mashindano ya Wimbledon yatakayoaanza Julai 3.

"Mpango ulikuwa kucheza Berlin, Eastbourne, na Wimbledon. Hakuna mashindano mengi duniani, lakini jambo la muhimu zaidi ni kurejelea katika afya nzuri."

Sorribes Tormo, aliyeorodheshwa wa 132 duniani, atakuwa akicheza katika wiki ya pili ya Grand Slam kwa mara ya kwanza.

Elena Rybakina ajiondoa kwenye mashindano ya French Open
Elena Rybakina ajiondoa kwenye mashindano ya French Open AP - Aurelien Morissard

Atamenyana na Ekaterina Alexandrova wa Urusi au Beatriz Haddad Maia wa Brazil kwa nafasi ya robo-fainali.

Baadaye Jumamosi, Swiatek nambari moja duniani atachuana na Wang Xinyu wa China aliye katika nafasi ya 80 na kutinga hatua ya 16 bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.