Pata taarifa kuu

PSG kucheza dhidi ya Al Nassr na Inter Milan katika mechi ya kirafiki Julai 25

NAIROBI – Paris Saint-Germain itacheza dhidi ya Al Nassr ya Cristiano Ronaldo na Inter Milan katika mechi za kirafiki za majira ya kiangazi huko Japan, mabingwa hao wa Ufaransa wamethibitisha Ijumaa.

PSG kucheza mechi za kirafiki nchini Saudi Arabia mwezi Juni
PSG kucheza mechi za kirafiki nchini Saudi Arabia mwezi Juni © AFP - FRANCK FIFE
Matangazo ya kibiashara

PSG walisafiri kwenda Japan kucheza dhidi ya vilabu vitatu vya ndani msimu uliopita wa joto ambapo  walilakiwa na umati wa mashabiki wao.

Mwaka huu watamenyana na Al Nassr ya Saudi mjini Osaka Julai 25 na klabu ya J-League Cerezo Osaka siku tatu baadaye.

Hata hivyo hakutakuwa na pambano kati ya Ronaldo na mpinzani wake wa zamani Lionel Messi wakati huu raia huyo wa Argentina akitarajiwa kuondoka PSG.

Lionel Messi anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu
Lionel Messi anatarajiwa kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu AP - Francois Mori

Watakamilisha ziara yao ya Japan dhidi ya Inter, ambao wanacheza na Manchester City katika fainali ya ligi ya mabingwa, kwenye uwanja wa Kitaifa wa Tokyo mnamo Agosti 1.

City, Bayern Munich na Celtic pia wametangaza kuwa watafanya ziara nchini Japan msimu huu wa joto.

PSG ilifanikiwa kutwaa taji la 11 la Ufaransa wiki iliyopita huku Messi akifunga katika sare ya 1-1 ugenini Strasbourg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.