Pata taarifa kuu

Vilabu vyenye thamani zaidi duniani kwa mujibu wa Forbes

NAIROBI – Klabu ya Manchester United ndio klabu yenye thamani kubwa zaidi katika ligi kuu ya Uingereza kwa mujibu orodha iliyochapishwa na tovuti ya biashara ya Forbes Jumatano ya wiki hii.

Klabu ya Manchester United ni ya pili kwa thamani duniani
Klabu ya Manchester United ni ya pili kwa thamani duniani © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Manchester United, yenye thamani ya $6bn (£4.8bn), ni ya pili kwenye orodha nyuma ya Real Madrid ya Uhispania $6.07bn - mara ya kwanza klabu mbili kuwa juu ya $6bn.

Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur na Arsenal pia wameingia 10 bora.

Thamani ya Forbes kwa Manchester United imeongezeka kwa asilimia 30 tangu mwaka jana.

Real Madrid ilishika nafasi ya kwanza kuanzia 2022 huku ikiongeza thamani yake kwa 19%, huku wapinzani wao Barcelona wakiwa katika nafasi ya tatu wakiwa wameongoza orodha hiyo mwaka 2021.

Real Madrid ndio ya kwanza kwa vilabu vyenye thamani zaidi duniani
Real Madrid ndio ya kwanza kwa vilabu vyenye thamani zaidi duniani © AFP / ANDER GILLENEA

Tangu Forbes waanze kuchapisha orodha ya timu zenye thamani kubwa zaidi za kandanda duniani mwaka 2004, ni Real Madrid na Manchester United pekee ndizo zimeorodheshwa katika tano bora kila mwaka.

Kwingineko, thamani ya Newcastle United imeongezeka kwa 51% hadi $794m kufuatia ununuzi wao unaoungwa mkono na Saudi Arabia na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Orodha ya vilabu wenye thamani kubwa zaidi dunaini kwa mujibu wa jarida la kibiashara la Forbes (Kumi bora)

1. Real Madrid - $6.07bn (£4.9bn)

2. Manchester United - $6bn (£4.8bn)

3.Barcelona - $5.51bn (£4.4bn)

4.Liverpool - $5.29bn (£4.2bn)

5. Manchester City - $4.99bn (£4bn)

6. Bayern Munich - $4.86bn (£3.9bn)

7. Paris St-Germain - $4.21bn (£3.4bn)

8. Chelsea - $3.1bn (£2.5bn)

9. Tottenham Hotspur - $2.8bn (£2.2bn)

10. Arsenal - $2.26bn (£1.8bn)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.