Pata taarifa kuu

Vipers wametinga fainali ya tatu mfululizo ya Kombe la Uganda.

NAIROBI – Na Paul Nzioki

Wachezaji wa klabu ya Vipers ya nchini Uganda
Wachezaji wa klabu ya Vipers ya nchini Uganda © Vipers sport club
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uganda Vipers SC wamefuzu kwa fainali ya Kombe la Stanbic Uganda hapo jana Jumanne baada ya kuwashinda Soltilo Bright Stars.

Licha ya kufungwa bao 1-0 juzi na Kavumba, Vipers maarufu kama Venoms wametinga fainali, ikiwa ni nafasi yao ya tatu mfululizo.

Vipers walishinda mchezo wa marudiano kwa mabao 4-0 kwenye uwanja wa St. Mary’s, Kitende na hivyo kutinga fainali hiyo kwa jumla ya mabao 4-1.

Bao pekee la mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Kavumba Recreation Centre lilifungwa na Nelson Ssenkatuka dakika ya 40.

Vipers ndiyo mabingwa wa ligi kuu nchini Uganda
Vipers ndiyo mabingwa wa ligi kuu nchini Uganda © Vipers sport club

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Vipers SC kwa mara ya tatu watatafuta kushinda mataji mawili kwa mara ya kwanza kabisa ya nyumbani.

Majaribio mawili ya awali mnamo 2018 na 2022 yameambulia patupu, na kupoteza katika fainali ya Kombe la Uganda kwa KCCA FC na BUL FC mtawalia.

The Venoms watamenyana na FUFA Big League Police FC ambao walikua bora zaidi ya Adjumani Town Council wakishinda kwa kanuni ya bao la ugenini.

Wachezaji wa klabu ya Vipers ya nchini Uganda wakiwa mazoezini
Wachezaji wa klabu ya Vipers ya nchini Uganda wakiwa mazoezini © Vipers sport club

Polisi walishinda mechi ya kwanza 1-0 wakiwa nyumbani kabla ya kupokea kichapo cha 2-1 kwenye Uwanja wa Pardi lakini walifuzu hadi fainali.

Fainali itachezwa Jumamosi hii (Juni 3, 2023) kwenye uwanja wa Akii Bua, Lira City.

Vipers pia ndio wawakilishi wa Uganda katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika Msimu ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.