Pata taarifa kuu

Mbappe ndiye mchezaji bora wa Ufaransa kwa mara ya nne mfululizo

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Kylian Mbappé, Mchezaji wa PSG
Kylian Mbappé, Mchezaji wa PSG REUTERS - PASCAL ROSSIGNOL
Matangazo ya kibiashara

Kylian Mbappe alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligue 1 msimu huu kwa mara ya nne mfululizo Jumapili baada ya kuisaidia Paris Saint-Germain kushinda rekodi ya taji la 11 la Ufaransa.

Nyota huyo wa Ufaransa amefunga mabao 28 kwenye ligi msimu huu na yuko mbioni kumaliza kama mfungaji bora wa ligi kwa msimu wa tano unaoendelea.

"Ni furaha, siku zote nilitaka kushinda, kuandika jina langu kwenye historia ya ligi. Lakini hata kwa matamanio yote niliyonayo sikutarajia kushinda haraka hivyo,” alisema Mbappe alipopokea tuzo yake.

Mbappe aliipiga chenga Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita na kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kusalia PSG.

Kylian Mbappé  wa Paris Saint-Germain
Kylian Mbappé wa Paris Saint-Germain REUTERS - STEPHANIE LECOCQ

Kulingana na ripoti, kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 itaisha mwaka ujao japokuwa anauwezo wa kuchagua kusalia hadi 2025.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake katika hafla ya tuzo hizo, Mbappe alijibu: "Nitakuwa hapa tena msimu ujao."Yeye ndiye mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo mara nne kwa mara ya kwanza mwaka 1994, akimpita Zlatan Ibrahimovic ambaye alishinda tuzo hiyo mara tatu akiwa na PSG.

Kylian Mbappé, Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa
Kylian Mbappé, Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa © YVES HERMAN/REUTERS

Franck Haise wa Lens alitawazwa kuwa kocha bora wa msimu huu baada ya kuiongoza klabu hiyo hadi nafasi ya pili na kurejea katika soka ya ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miongo miwili.

Kipa wa Lens Brice Samba pia alitunukiwa huku beki wa kushoto wa Paris Saint-Germain Nuno Mendes akipata tuzo ya mchezaji bora chipukizi.

Nuno Mendes wa PSG.
Nuno Mendes wa PSG. © AFP - FRANCK FIFE

Alikuwa mmoja wa wachezaji wanne wa PSG katika timu ya msimu pamoja na Mbappe, Lionel Messi na Achraf Hakimi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.