Pochettino ndiye kocha mpya wa Chelsea
NAIROBI – Chelsea imemtangaza rasimi Mauricio Pochettino kuwa kocha wake mpya, kibarua anachokichukua wakati huu klabu hiyo ikiandikisha matokeo duni msimu uliopita.
Imechapishwa:
Pochettino amekubali kandarasi ya miaka miwili ambapo mkataba huo unaweza kuongezwa kwa mwaka mmoja kwa makubaliano ya pande hizo mbili.
Kocha huyo anarejea katika ligi kuu ya Uingereza miaka minne baadae baada ya kufutwa na mahasimu wa Chelsea jijini London Tottenham.
Pochettino mwenye umri wa miaka 51 hajakuwa na ajira tangu kutimuliwa na Paris Saint-Germain ya Ufaransa mwezi Julai mwaka wa 2022.
Chelsea Football Club is pleased to announce Mauricio Pochettino as the club’s new head coach!
— Chelsea FC (@ChelseaFC) May 29, 2023
Kocha huyo anatarajiwa kuaanza majukumu rasimi tarehe moja ya mwezi Juali, akichukua nafasi ya Frank Lampard amabye amekuwa akiitumikia Chelsea kama kocha wa muda hadi kumalizika kwa msimu.
Lampard alikuwa meneja wa tatu wa Chelsea baada ya mmiliki wa klabu hiyo Boehly kumtimua Thomas Tuchel mnamo Septemba na kisha kumfuta mrithi wake Graham Potter mwezi Aprili baada ya kipindi cha miezi saba.
Pochettino aliibuka kidedea baada ya Chelsea kufanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania Luis Enrique na Julian Nagelsmann, ambaye alitimuliwa na Bayern Munich mwezi Machi.
Mauricio alikubali kuchukua mikoba ya kuinoa Chelsea mwezi Aprili, lakini uteuzi huo ukasitishwa hadi mwisho wa msimu.
Pochettino anakuja Stamford Bridge wakati huu ambapo The Blues wanakabiliwa na wakati mgumu ambapo wamemaliza katika nafasi ya 12 msiumu uliomalizika, nafasi wanayoshikilia tangu mwaka wa 1996.