Pata taarifa kuu

Soka: Mosimane aendelea kupata mafanikio kama kocha

NAIROBI – Na Jason Sagini

 Pitso Mosimane.
Pitso Mosimane. REUTERS - JUAN MEDINA
Matangazo ya kibiashara

Kocha wa zamani wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane ameiongoza klabu yake ya Al Ahli kutoka nchini  Saudi Arabia kutwaa ubingwa wa Ligi ya daraja la kwanza nchini humo kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al-Qadisiyah FC.  

Ushindi huo umeifanya Al Ahli kufikisha pointi 71 kwenye msimamo wa ligi na kujihakikishia ubingwa na kufuzu ligi kuu msimu ujao baada ya wapinzani wake wa karibu Al Akhdood wenye alama 65 kupokea kichapo cha 3-2 dhidi ya Al Sahel SC na kushuka hadi nafasi ya tatu huku Al Hazem FC yenye alama 67 ikikwea mpaka nafasi ya pili. 

Mosimane aliichukua Al Ahli ikiwa nafasi ya tano na kuiongoza kushinda mechi 18, sare 6 na vipigo vitatu na kuipandisha daraja kwenda Ligi kuu ya Saudi Pro sambamba na kutwaa ubingwa huo wa kihistoria. Mosimane ametwaa kombe lake la 19 katika maisha yake ya ukocha likiwa ni kombe lake la kwanza akiwa nje ya Afrika. 

Pitso raia wa Afrika Kusini, akiwa na SuperSport United ya nchini humo alishinda taji la Super Eight na kombe la Nedbank.

Kocha Pitso Mosimane.
Kocha Pitso Mosimane. AFP - KARIM JAAFAR

Mosimane pia alipata mafanikio makubwa akiwa Mamelodi Sundowns baada ya kushinda mataji matano ya Ligi kuu ya Afrika Kusini, mataji mawili ya Nedbank na mengine mawili ya Telkom Knockouts, Ligi ya Mabingwa Afrika mara moja mwaka 2016 na CAF Super Cup mara moja.  

Akiwa na klabu ya Al Ahly ya Misri, Mosimane alishinda Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili, CAF Super Cup mara mbili sambamba na kombe la ligi kuu ya Misri mara moja. 

Licha ya mafanikio hayo inaelezwa kuwa klabu ya Al Ahli Jeddah haipo tayari kumuongeza mkataba mpya huku ikidaiwa ipo sokoni kutafuta kocha mwingine atakayeinoa klabu hiyo kwenye Saudi Pro League msimu ujao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.