Pata taarifa kuu

Rwanda: Habyarimana apewa wadhifa wa muda kuongoza Ferwafa

NAIROBI – Wajumbe wa shirikisho la soka nchini Rwanda Ferwafa, wamempa kazi Marcel Matiku Habyarimana kuchukua jukumu la kuliongoza shirikisho hilo kwa muda hadi atakapochaguliwa kuwa bosi mpya wa Tarehe 24 mwezi Juni.

Shirikisho la soka nchini Rwanda Ferwafa
Shirikisho la soka nchini Rwanda Ferwafa Ferwafa
Matangazo ya kibiashara

Habyarimana, ambaye alikuwa akihudumu kama makamu wa rais wa shirikisho, aliidhinishwa wakati wa mkutano mkuu uliofanyika faragha mjini Kigali siku ya Jumatatu.

Anachukua hatamu kufuatia kujiuzulu kwa rais anayemaliza muda wake Olivier Mugabo Nizeyimana ambaye aliondoka madarakani Aprili 19, akitaja sababu za kibinafsi ikiwa ni pamoja na kile alichokitaja kuwa "kazi nyingi."

Katika Kikao hicho pia, mwenyekiti na mmiliki wa Gorilla FC Hadji Yussuf Mudaheranwa na rais wa Inyemera WFC Ancille Mukankaka wamechaguliwa kumsaidia Habyarimana kuongoza kamati ya utendaji katika muda wote wa muda wa siku 39.

Kamati ya uchaguzi ikiongozwa na Adolphe Kalisa pia iliwafahamisha wanachama wa shirikisho hilo ajenda ya uchaguzi wa Ferwafa.

Wakati wa uchaguzi ujao, mkutano mkuu utajaza nafasi zilizoachwa wazi na wajumbe wa kamati hiyo waliojiuzulu mwezi mmoja uliopita akiwemo rais wa zamani Olivier Nizeyimana Mugabo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.