Pata taarifa kuu

Tanzania: Joash Onyango 'Babu' aashiria kuondoka Simba

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Joash Onyango ameshiria kuwa huenda akaondoka katika klabu ya Simba ya nchini Tanzania
Joash Onyango ameshiria kuwa huenda akaondoka katika klabu ya Simba ya nchini Tanzania © simba
Matangazo ya kibiashara

Beki wa kimataifa wa Kenya anayecheza katika klabu ya Simba ya Tanzania, Joash Onyango huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho katika klabu hiyo.

Onyango tayari ameuomba uongozi wa simba kukubali ombi lake la kuvunja mkataba na kuacha kuwatumikia wekundu wa msimbazi.

Beki huyo alijiunga na klabu ya simba mwezi Agosti  tarehe 14 mwaka 2020 akitokea Gor Mahia ya Kenya akisaini mkataba wa miaka miwili.

Onyango alijunga na Simba akitokea katika klabu ya Gor Mahia ya Kenya
Onyango alijunga na Simba akitokea katika klabu ya Gor Mahia ya Kenya © FMM

Hata hivyo Onyango maarufu kama BABU kwa jina la utani amewatumikia wekundu wa msimbazi kwa mafanikio makubwa katika mechi za ligi kuu Tanzania Bara lakini vilevile kwenye michuano ya CAF na baadaye kuongezwa mwaka mmoja unaotarajia kumalizika msimu ujao.

Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na gazeti moja la michezo nchini Tanzania, taarifa za ndani kutoka Simba zilieleza kuwa mchezaji huyo kutokana na lawama za mara kwa mara anazopewa kila anapofanya makosa uwanjani na mashabiki ameomba kumalizana nao ili aondoke.

Onyango tayari ameuomba uongozi wa simba kukubali ombi lake la kuvunja mkataba wake
Onyango tayari ameuomba uongozi wa simba kukubali ombi lake la kuvunja mkataba wake © simba

"Wachezaji ni wengi ambao hawana furaha ndani ya Simba, sasa lakini Onyango ameona isiwe shida kwa kuamua kuandika barua ya kuomba kuondoka hilo lipo chini ya viongozi wanalijadili.

"Tunaweza tusiwe naye msimu ujao kwasababu hata viongozi pia walikuwa wanamtafutia sababu ili kumuondoa kikosini, hivyo kwasababu yeye mwenyewe kaomba kuondoka msimu ukiisha utaratibu utafanyika." Liliandika gazeti la mwanaspoti.

Aidha Simba wanatambua mchango wa mchezaji huyo ndani ya klabu na kuamini kuwa mchezo wa soka una vitu vingi hivyo hawana budi kumpa nafasi ya kuondoka ili kuondoa changamoto iliyopo ya kuangushiwa mzigo kila timu inapopata matokeo mabaya.

Hata hivyo Onyango amekana taarifa hizo baada ya majarida kadhaa ya Tanzania kumtafuta ili kuweka wazi ukweli kuhusu taarifa hizo.

Joash Onyango ameonekana amekuwa akiichezea Simba tangu kuondoka Gor Mahia
Joash Onyango ameonekana amekuwa akiichezea Simba tangu kuondoka Gor Mahia © simba

Onyango amesema yeye kama mchezaji hawezi kuzungumzia hilo.

"Siwezi kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo kama lipo na viongozi ndio watu sahihi wa kulizungumzia lakini mimi siwezi kuwa na jibu kuhusiana na mambo ambayo yamekuwa yakizushwa na watu.

"Tanzania kumekuwa na kawaida ya watu kuandika vitu ambavyo hawana uhakika navyo na kuvisambaza kama umesikia mitandaoni siwezi kulizungumzia suala hilo na kama lipo watu sahihi wa kulizungumzia ni viongozi." alisema.

Onyango amekua muhimili mkubwa katika safu ya Ulinzi ya Simba akiwasaidia kutwaa taji moja akijumuishwa katika kikosi cha kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.