Pata taarifa kuu

Rwanda: APR na Ryon Sports zinatafuta tiketi ya kucheza klabu bingwa Afrika

NAIROBI – Mwenyekiti wa Club ya APR Luteni Jenerali Mubaraka Muganga, akiongea na RFI, amesema timu yao ina mtihani mgumu wakati huu kufuatia wachezaji 4 katika safu ya ulinzi, wana majeraha.

Timu za Rwanda ,APR na Rayon sports zinashindana kuwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya CAF klabu bingwa Afrika
Timu za Rwanda ,APR na Rayon sports zinashindana kuwakilisha nchi hiyo katika mashindano ya CAF klabu bingwa Afrika © Courtesy of CAF
Matangazo ya kibiashara

Hatukufanya vizuri sana kama ilivyotarajiwa kwa sababu walinzi wetu watatu wamejeruhiwa.” amesema Mwenyekiti wa Club ya APR Luteni Jenerali Mubaraka Muganga

00:39

Mwenyekiti wa Club ya APR Luteni Jenerali Mubaraka Muganga

Kutotumia wageni katika club hii ya APR imekuwa changamoto wakati timu zingine zikiruhusiwa kutumia wachezaji watano.  

Hii ikiwa sera ya timu hiyo ya kutotumia wageni hadi pale watakapotwaa ubingwa msimu huu.

Minani Hemedi ni Kiongozi wa mashabiki wa Kiyovu sports Club ametoa hamasa   kwa mashabiki wake

Lengo letu hasa tunachunguza mechi kwa mechi, tunakwenda kupambana na Sunarise, kwa bahati nzuri na sala za wanyarwanda, hili kombe tutalibeba.” amesema Minani Hemedi ni Kiongozi wa  mashabiki wa Kiyovu sports  Club

00:11

Minani Hemedi ni Kiongozi wa mashabiki wa Kiyovu sports Club

Kocha  wa Gorilla FC Gatera Mussa ambaye, anatathmini  kuhusu vigogo hao  wanaoendelea kusaka taji la ubingwa.

“Labda timu ngumu ambayo APR imebaikia nayo ni AC Kigali bado mechi ya mwisho wanaweza wakateleza, kubeba ubingwa inakuwa ngumu.” amesema Kocha  wa Gorilla FC Gatera Mussa.

00:15

Kocha wa Gorilla FC Gatera Mussa

Mpaka sasa  Kiyovu wanaongoza ligi na alama 60, Apr wanashikilia nafasi ya 2 na alama 57 huku Rayon ikiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye jedwari na alama 55.

Espoir FC ya Rusizi wao tayari wameshuka daraja la pili.

Timu bingwa wa ligi kuu huwakilisha Rwanda katika kombe la mabingwa barani (Africa CAF Champions League) wakati  mabingwa wa kombe la Amani huwakilisha  Kombe la  Shirikisho barani Afrika (CAF Confederaton Cup).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.