Pata taarifa kuu

PSG inaweza kuibuka bingwa wa  Ligue 1

NAIROBI – Uchambuzi wa Paul Nzioki

Wachezaji wa PSG
Wachezaji wa PSG © AFP / NICOLAS TUCAT
Matangazo ya kibiashara

Paris Saint-Germain ni klabu iliyokumbwa na msukosuko. Kocha Christophe Galtier amekuwa  chini ya shinikizo , kusimamishwa kwa Lionel Messi na maandamano ya mashabiki nje ya nyumba ya Neymar miongoni mwa changamoto zingine. 

Msimu huu tayari, PSG inaonekana kushuka viwango baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa bara Ulaya na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora na kutolewa katika Kombe la Ufaransa katika hatua hiyo hiyo. 

Bayern waliwaondoa Paris St Germain katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya
Bayern waliwaondoa Paris St Germain katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya REUTERS - ANGELIKA WARMUTH

Licha ya kuwa  kileleni mwa Ligue 1, wakiwa na alama  tano mbele ya Marseille zikiwa zimesalia mechi tano. Je, wako tayari kutetea taji na kuwa mabingwa wa Ufaransa kwa mara ya 11? kampeni hiyo inaonekana kua na maswali mengi kuliko majibu. 

Kipigo cha pili wiki iliyopita cha mabao 3-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Lorient kinamaanisha kuwa timu hiyo ya Galtier imepoteza mechi sita kati ya 17 za Ligue 1 mnamo 2023, hali ambayo ni mbaya kwa timu ambayo haikupoteza mchezo wowote katika mashindano yoyote kabla ya Kombe la Dunia. 

Siku moja baada ya kupoteza kwa Lorient, Messi hakufika mazoezini, badala yake alisafiri kwenda Saudi Arabia bila ruhusa ya PSG kutimiza ahadi kama sehemu ya mkataba na ofisi ya utalii ya nchi hiyo. 

Lionel Messi anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain kuelekea Saudi Arabia
Lionel Messi anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain kuelekea Saudi Arabia REUTERS - SARAH MEYSSONNIER

Mshindi huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d’Or tangu wakati huo amesimamishwa na klabu hiyo na anatazamiwa kutocheza wikendi hii dhidi ya Troyes. 

Kwa vyovyote vile, kocha Christophe Galtier anaonekana kuwa na uwezekano wa kuwa na kibarua chake bado msimu ujao huku mabadiliko makubwa yakitarajiwa katika msimu wa joto. 

Mamia ya mashabiki waliandamana Jumatano nje ya ofisi za klabu hiyo na pia mbele ya nyumba ya Neymar katika kitongoji cha Paris cha Bougival. 

"Tumetosha mamluki," waliimba. 

Christophe Galtier kocha wa PSG
Christophe Galtier kocha wa PSG REUTERS - ANGELIKA WARMUTH

PSG ilipuuzilia mbali matukio hayo kama "vitendo visivyovumilika na vya matusi vya kikundi kidogo cha watu binafsi", lakini yote yanaongeza hisia za klabu kuwa mkanganyiko. 

Wapinzani wao wa karibu, na Marseille, timu mbili za kuvutia zinazocheza na PSG, zitamenyana wikendi hii. 

Kylian Mbappé wa PSG wakati wa mechi yao ya Ligue 1 dhidi ya Lens awali
Kylian Mbappé wa PSG wakati wa mechi yao ya Ligue 1 dhidi ya Lens awali © AFP / ANNE-CHRISTINE POUJOULAT

Kipaumbele cha wote wawili ni kupata nafasi ya pili na kufuzu moja kwa moja kwenye Ligi ya Mabingwa. 

Wapinzani wawili wanaofuata wa PSG - wanacheza na Ajaccio baada ya kukabiliana na Troyes na wote wana uhakika wa kushuka daraja. 

Je,PSG hii iliyojikwaa tayari na mikosi ya kuwaajiri mastaa wenye mishahara mikubwa, Hao hao mastaa hawana taji la klabu bingwa, Psg iliyojaa mizozo, licha ya kila kitu, wtakuwa mabingwa wa Ligue 1 tena? 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.