Pata taarifa kuu

Lionel Messi kucheza nchini Saudi Arabia msimu ujao

NAIROBI – Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, atacheza nchini Saudi Arabia msimu ujao, kwa mujibu wa mtu wa karibu katika mazungumzo yanayoendelea kufanyika kati ya mchezaji huyo na wawakilishi kutoka Saudia.

Lionel Messi kucheza nchini Saudia Arabia msimu ujao
Lionel Messi kucheza nchini Saudia Arabia msimu ujao AP - Francois Mori
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu na mazungumzo hayo, Messi anatarajiwa kupewa mkataba mzuri ambao  kwa sasa unaendelea kukamilisshwa.

Klabu ya PSG kwa upande imesema inatambua kuwa mkataba wa mchezaji huyo ambaye kwa sasa bado ni mchezaji wao unakamilika tarehe 30 ya mwezi Juni.

Taarifa nyengine kutoka kwa mtu wa karibu na PSG imeeleza kuwa iwapo klabu hiyo ingekuwa na nia ya kurefusha mkataba wa Messi ingelifanya hivyo mapema.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, mshindi wa kombe la dunia na klabu yake ya Argentina alipewa adhabu ya kutoshirki mechi kadhaa na klabu yake kwa kile kilitajwa kuwa alifanya ziara nchini Saudi bila ya ruhusa ya klabu.

Mechi anaelekea nchini Saudia ambapo Cristiano Ronaldo wa Ureno anacheza katika klabu ya Al Nassr tangu mwezi Januari.

Ronaldo anadiwa kulipwa euro milioni 400 katika mkataba huo unaokamilika Juni mwaka wa 2025 ambapo anatajwa kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.