Pata taarifa kuu

Ufaransa: Lorient yaiduwaza PSG kwa kipigo cha 3-1

NAIROBI – Lorient inayoshiriki katika ligi kuu ya Ufarasna iliishinda Paris Saint-Germain 3-1 katika mechi iliyosakatwa uwanjani Parc des Princes baada ya viongozi hao wa Ligue 1 kupunguzwa hadi wachezaji 10 baada ya Achraf Hakimi kuonyeshwa kadi nyekundu mapema katika kipindi cha kwanza. 

Wachezaji wa PSG baada ya kipigo cha 3-1 dhidi ya Lorient katika mechi ya Ligue 1
Wachezaji wa PSG baada ya kipigo cha 3-1 dhidi ya Lorient katika mechi ya Ligue 1 AP - Aurelien Morissard
Matangazo ya kibiashara

PSG, ambao sasa wamepoteza mechi tisa katika mashindano yote mwaka huu, wamesalia na alama 75 baada ya  mechi 33 na uongozi wao wa Ligue 1 huenda ukapunguzwa kwa alama tano ikiwa Marseille wataifunga Lens katika mechi ijayo ya Jumapili.  

Lorient ilichukua uongozi katika dakika ya 15 kupitia kwa Enzo Le Fee ambaye alipokea pasi yake Romain Faivre. 

Masaibu ya PSG yaliongezeka dakika tano baadaye baada ya Hakimi kupatiwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea vibaya Darline Yongwa, kabla ya Kylian Mbappe kusawazisha katika mazingira ya kutatanisha kufuatia makosa ya kipa Yvon Mvogo.

Wachezaji wa Lorient  baada ya ushindi wao wa 3-1 dhidi ya PSG katika mechi ya Ligue 1
Wachezaji wa Lorient baada ya ushindi wao wa 3-1 dhidi ya PSG katika mechi ya Ligue 1 REUTERS - CHRISTIAN HARTMANN

Mvogo aliokoa mpira na kujaribu kuanza tena mchezo lakini mpira ukamgonga Mbappe ambaye alikuwa akirudi nyuma karibu naye, Mbappe aliuchukua na kuutia wavuni. 

Bao la pili la Lorient lilipatikana wakati Faivre alipocheza tiki taka na kupatia Yongwa pasi, na kufanya matokeo kuwa 2-1. 

Lorient ilichukua uongozi katika dakika ya 15 kwa mwingiliano nadhifu kwenye upande wa kulia wa safu ya ulinzi ya PSG, na kumruhusu Romain Faivre kuuweka mpira kwenye eneo la hatari ambapo Enzo Le Fee alipiga shuti ambalo liliwafurahisha mashabiki wa Lorient. 

Lionel Messi wa PSG
Lionel Messi wa PSG AP - Aurelien Morissard

Hali ilikuwa mbaya kwa timu ya nyumbani huku wachezaji wa PSG wakizidi kuzomewa na kukejeliwa na mashabiki wa nyumbani, walijaribu kwa kila juhudi kupata bao la kusawazisha huku Sergio Ramos akiunganisha mpira wa kichwa kwa Lionel Messi, lakini mlinda lango wa Lorient Mvogo akiokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Danilo Pereira kwa kichwa.

Sergio Ramos wa PSG wakati wa mechi ya Ligue 1 kati ya PSG dhidi ya Lorient
Sergio Ramos wa PSG wakati wa mechi ya Ligue 1 kati ya PSG dhidi ya Lorient AP - Aurelien Morissard

Bamba Dieng alifunga bao la dakika za lala salama lakini lilikataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea lakini dakika moja baadaye akafunga bao la tatu la Lorient na kuhakikisha kuwa timu yake imetia alama tatu mfukoni. 

Kutokana na matokeo hayo PSG bado inashikilia nafasi ya kwanza na alama 75 baadaya mechi 33. Marseille ni ya pili ikiwa na alama 70 nayo Lens inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na alama 66 baada y mechi 32. Lorient ni ya kumi ikiwa na alama 48. 

Matokeo ya jana 

Monaco 0-4 Montpellier 

Clermont 1-0 Reims 

Rennes 4-2 Angers 

Troyes 0-1 Nice 

PSG 1-3 Lorient 

Marseille 2-1 Auxerre  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.