Pata taarifa kuu

Morocco: Uchunguzi umeanzishwa baada ya shabiki kufariki nje ya uwanja Mohammed V

Nairobi – Mamlaka ya Morocco imeanza uchunguzi baada ya shabiki kufariki dunia nje ya uwanja kabla ya mechi ya Raja Casablanca dhidi ya Al Ahly.

Mashabiki wa Raja Casablanca wakiwasha moto katika mechi ya kirafiki kati ya Roma na Raja Casablanca, katika uwanja wa Olympic Stadium, Jumamosi, Agosti. 14, 2021.
Mashabiki wa Raja Casablanca wakiwasha moto katika mechi ya kirafiki kati ya Roma na Raja Casablanca, katika uwanja wa Olympic Stadium, Jumamosi, Agosti. 14, 2021. AP - Andrew Medichini
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka mjini Casablanca imeanzisha uchunguzi baada ya shabiki mmoja kufariki nje ya lango la Uwanja wa Stade Mohammed V kabla ya mechi ya Raja Casablanca dhidi ya Al Ahly katika mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Shabiki huyo, mwanamke mwenye umri wa miaka 29, alifariki dunia katika mtanange huo Jumamosi wakati maelfu ya mashabiki wakijaribu kuingia uwanjani kutazama mechi ambayo Raja Casablanca ilikuwa ikijaribu kupindua matokeo ya mabao 2-0 kutoka kwa mkondo wa kwanza nchini Misri.

“Aziz El Badrawy, Rais wa Al-Raja Club Athletic, kwa jina lake na kwa niaba ya wanachama wote wa klabu, anatoa pole kwa familia ya shabiki, Noura, aliyefariki kabla ya mechi ya timu yetu dhidi ya Al-Ahly. ,” klabu ya Morocco ilisema katika taarifa.

Katika hatua nyingine, robo fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa wa CAF kati ya Esperance na JS Kabylie ya Algeria mjini Tunis ilikumbwa na machafuko ya mashabiki, ambayo ilisababisha mechi kuchelewa kwa dakika 40 katika kipindi cha pili.

Mashabiki wa Esperance walipambana na vikosi vya usalama vya Tunisia na kuwasha fataki wakati wa mapumziko kwenye Uwanja wa Rades. Wazima moto walilazimika kuitwa kuzima mioto uwanjani

Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1, lakini Esperance walitinga nusu fainali kwa jumla ya 2-1 baada ya ushindi wa 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Watamenyana na Al Ahly katika mechi mbili za kufuzu fainali baada ya klabu hiyo ya Cairo kuishinikiza Raja kwa sare ya 0-0 mjini Casablanca.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.