Pata taarifa kuu

Italia: Sherehe za ubingwa wa Napoli zimesitishwa kwa muda baada ya kutoka sare na Salernitana

Nairobi – Napoli wangeshinda taji lao la kwanza la Serie A tangu 1990 ikiwa wangewashinda wapinzani wao katika mechi ya jana.

Napoli ikishereheka ushindi katika mechi ya kundi A Klabu bingwa barani Ulaya dhidi Ya Liverpool.
Napoli ikishereheka ushindi katika mechi ya kundi A Klabu bingwa barani Ulaya dhidi Ya Liverpool. AP - Andrew Medichini
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Napoli ambayo inashiriki ligi kuu nchini Italia italazimika kusubiri angalau siku nne zaidi kutwaa ubingwa wa ligi ya Serie A baada ya kutoka sare ya 1-1 na wapinzani wao Salernitana, jambo lililowakatisha tamaa mashabiki wa klabu hiyo ambao tayari walikuwa wameanza kusherehekea kwa kutarajia ubingwa.

Partenopei wangeweza kushinda ubingwa wa ligi huku zikiwa zimesalia mechi sita ikiwa wangeifunga Salernitana katika mechi ya Jumapili, lakini Boulaye Dia alisawazisha wageni dakika sita kabla ya mechi kumalizika baada ya Mathias Olivera kuifungia Napoli bao la kufunguzi.

Matokeo hayo yamewaacha vinara Napoli wakiwa na alama 18 mbele ya Lazio iliyo nafasi ya pili, ambao walipoteza 3-1 dhidi ya Inter Milan.

Juventus walio nafasi ya tatu wanaweza kuiruka Lazio na kushika nafasi ya pili iwapo watashinda Bologna.

Napoli inapania kushinda ligi ya Italia kwa mara ya kwanza tangu Diego Maradona alipoongoza klabu hiyo kutwaa mataji yake mawili ya Serie A mwaka 1987 na 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.