Pata taarifa kuu

Michuano ya CHAN baina ya vijana kuanza nchini Algeria

Na: Jason Sagini

Makundi ya michuano ya CHAN kwa vijana wasiozidi miaka 17 nchini Algeria
Makundi ya michuano ya CHAN kwa vijana wasiozidi miaka 17 nchini Algeria © CAF_Online
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya pili chini ya miezi mitatu, taifa la Algeria litafungua milango yake tena kukaribisha bara zima kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 baada ya kuandaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2023 kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani maarufu CHAN. 

Timu 12 zimejiandaa vilivyo kushindania ubingwa pamoja pia na kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la dunia la mwaka huu kwa wachezaji wasiozidi miaka 17. Jiji la Algiers, Annaba na Constantine ndizo zitahusika kwa mashindano haya.  

Hii ni mara ya tano katika historia taifa la Algeria kuandaa mashindano ya bara Afrika na mara ya pili kuandaa mashindano ya chipukizi wasiozidi miaka 17 baada ya kuandaa mara ya kwanza mwaka 2009.

Algeria pia iliandaa na kushinda kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 1990 na walikua waandalizi wa mashindano hayo kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 mwaka 2013. 

Mashabiki na wenyeji wa Algeria wameonesha furaha kubwa ya kuandaa na kushuhudia soka la Afrika. 

 “Tunatarajia kuona ikianzia hapa sababu ni furaha kubwa kufika uwanjani na kukaribisha Afrika nzima,” alisema Mohamed raia katika jiji la Annaba. 

Anaongeza kwa kusema kuwa, “Tuliandaa CHAN kwa mafanikio makubwa na kila mtu aliona yalikuwa mashindano bora kabisa ya CHAN katika historia. Matumaini yetu ni kuwa tutaandaa mashindano zaidi sababu Algeria ni taifa bora Afrika kwenye soka.” 

Jijini Constantine, barabara zote zimerembeshwa kwa bendera za mataifa yote 12 na mabango ya mashindano, hili likiashiria mashindano kuwadia kuanza rasmi.

Hata sura za wafanyakazi katika uga wa Mohammed Hamlaoui, wenye uwezo wa kubeba mashabiki elfu 23, zimeripotiwa kujaa tabasamu  

Matumaini ya mashabiki wa Algeria ni kuwa wataandaa mashindano haya vizuri na kulitwaa taji haswa baada ya kupoteza kwenye fainali ya kombe la CHAN dhidi ya Senegal mwezi Januari. 

Cameroon ndio mabingwa watetezi wa mashindano haya ikiwa miongoni mwa mataifa tano pamoja na Gambia, Ghana, Mali na Nigeria yaliyonawiri zaidi kwenye mashindano haya – kila mmoja akiwa ameshinda kombe hili mara mbili. 

Mechi ya ufunguzi itachezwa leo usiku na itakutanisha wenyeji Algeria na katika uwanja wa  Stade de Nelson Mandela huko Baraki jijini Algiers 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.