Pata taarifa kuu

Chelsea wanakaribia kumteua Mauricio Pochettino kama Kocha Mkuu

NAIROBI – Chelsea wanakaribia kumteua aliyekua kocha wa zamani wa Paris Saint Germain Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mkuu.  

Mauricio Pochettino, Kocha wa zamani wa Tottenham
Mauricio Pochettino, Kocha wa zamani wa Tottenham AP - Rui Vieira
Matangazo ya kibiashara

Pochettino ndiye kocha anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kupewa ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu na inaripotiwa kuwa kuna ongezeko la mazungumzo ya ambayo huenda yakafanikiwa.

Meneja huyo wa zamani wa Tottenham, ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka Paris Saint-Germain msimu uliopita, amepewa nafasi hiyo kubwa haswa baada ya Julian Nagelsmann kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho mwishoni mwa juma lililopita. 

Pochettino amefanya mfululizo wa mazungumzo na wamiliki wa Chelsea na inafahamika kwamba uthibitisho wa raia huyo wa Argentina kuwa  mrithi wa kudumu wa Graham Potter unaweza kuja hivi karibuni.

Graham Potter, aliyekuwa kocha wa Chelsea
Graham Potter, aliyekuwa kocha wa Chelsea AFP/File

Imesisitizwa, hata hivyo, kwamba mpango huo haujakamilika na kwamba klabu hiyo inawazia kuhusu wagombea wengine iwapo mazungumzo kati yake na Pochettino yatavunjika.  

Wamiliki wenza wa Chelsea, Todd Boehly na Behdad Eghbali, wako chini ya shinikizo la kufanya uteuzi sahihi baada ya timu kuendelea kupata matokeo yasiyo mazuri chini ya mkufunzi wa muda Frank Lampard ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Chelsea.

Chelsea ilimpa Frank Lampard  majukumu ya muda baada ya kumfuta kazi Potter mwezi huu. 

Frank Lampard, Kocha wa muda wa Chelsea
Frank Lampard, Kocha wa muda wa Chelsea AFP/File

Pochettino, ambaye uhusiano wake na Spurs hauwezekani kuwa kizuizi kwa kuchukua kazi hiyo, atakuwa meneja wa tatu wa kudumu kufanya kazi chini ya umiliki huu mpya iwapo atapewa kazi hiyo.  

Potter, ambaye alikuwa kwenye wadhifa huo kwa miezi saba pekee, aliletwa baada ya kutimuliwa kwa Mjerumani Thomas Tuchel Septemba iliyopita ambaye kwa sasa ndiye kocha wa Bayern Munich. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.