Pata taarifa kuu

Pochettino anapewa nafasi kubwa kuinoa Chelsea baada ya Nagelsmann kujiondoa

NAIROBI – Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwa meneja ajaye wa Chelsea, baada ya Julian Nagelsmann kuripotiwa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Mauricio Pochettino, Kocha wa zamani wa Tottenham
Mauricio Pochettino, Kocha wa zamani wa Tottenham AP - Rui Vieira
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya mashabiki wa Spurs wamekuwa wakimtaka Pochettino arejee katika klabu hiyo ambayo aliipeleka kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019.

Hata hivyo, raia huyo wa Argentina ameripotiwa kuwa katika mazungumzo na wapinzani wao wa London, Chelsea, ambao wamekabiliwa na  msimu mbaya na kwa sasa.

The Blues tayari wamewatimua makocha wawili peke msimu huu baada ya kuwatimua Thomas Tuchel na Graham Potter na kwa sasa wananolewa na kocha wa muda, mchezaji wa zamani Frank Lampard.

Kocha wa muda Frank Lampard, ambaye amepoteza mechi zote nne tangu ateuliwe wiki mbili zilizopita, bado anatarajiwa kuinoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Meneja wa Burnley Vincent Kompany pia ni miongoni mwa majina yanayotarajiwa  kuteuliwa kuwa meneja wa Chelsea.

Kompany ameongoza klabu yake ya Burnley kurejea Ligi Kuu mara moja msimu huu na watatawazwa washindi wa Ubingwa kwa ushindi dhidi ya QPR Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.