Pata taarifa kuu

Marcus Rashford kukosa mechi kadhaa za United kutokana na jeraha

NAIROBI – Klabu ya Manchester United imethibitisha kuwa mchezaji wake Marcus Rashford atakosa mechi ya robo fainali kuwania ubingwa wa ligi ya Europa dhidi ya Sevilla kutokana na jeraha la misuli.

Marcus Rashford wa Manchester United
Marcus Rashford wa Manchester United Reuters/Carl Recine
Matangazo ya kibiashara

Rashford mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameifungia United magoli 28 msimu huu, aliondoka uwanjani akichechemea wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Everton wikendi iliyopita, mechi waliopata ushindi wa 2-0.

"Marcus Rashford hatakuwepo kwenye mchezo wa Alhamisi wa robo fainali ya UEFA Europa League dhidi ya Sevilla kwa sababu ya jeraha la misuli," United ilisema kwenye taarifa yake.

Wakati wa mechi hiyo ya ligi kuu ya Uingereza, mshambuliaji huyo wa United, aliondolewa nje ya uwanja katika dakika ya 80 na akaelekea moja kwa moja kupata matibabu ya jereha hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zaidi kutoka kwa klabu yake, mchezaji huyo huenda akakosa mechi zengine kadhaa kando na mechi dhidi ya Sevila.

United wamepigwa jeki na kurejea kwa Anthony Martial ambaye amekuwa akiuuguza jeraha, Martial alifanikiwa kupata bao dhidi ya Everton.

Kiungo mbunifu Christian Eriksen alirejea kutoka katika jeraha la muda mrefu kama mchezaji wa akiba dhidi ya Everton huku United wakitarajiwa kumkaribisha Casemiro katika kikosi cha Alhamisi dhidi ya Sevilla baada ya kiungo huyo wa Brazil kutumikia adhabu ya kutocheza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.